Filtra per genere

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

RFI Kiswahili

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.

293 - Mazishi ya wakimbizi wa ndani 35 DRC, Uganda na Kenya zaimarisha mapatano yao
0:00 / 0:00
1x
  • 293 - Mazishi ya wakimbizi wa ndani 35 DRC, Uganda na Kenya zaimarisha mapatano yao

    Baadhi ya mambo tunayoangazia ni mazishi ya watu 35 waliouawa baada ya bomu kulipuka katika kambi ya wakimbizi wa ndani eneo la Mugunga nje kidogo ya jiji la Goma, suala la Uingereza kuwahamisha wahamiaji huko Rwanda, ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Kenya, siasa za Sudan na eneo la Afrika Magharibi, pia huko Ulaya na Marekani

    Sat, 18 May 2024
  • 292 - Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yamerejelewa jijini Nairobi, Kenya

    Katika makala ya wiki hii baadhi ya matukio ya ulimwengu tutakayoangazia ni mazungumzo ya kutafuta amani nchini Sudan Kusini ambayo yalianza Alhamisi jijini Nairobi, lakini pia madaktari nchini Kenya kusitisha mgomo wa siku 56, vilevile kule DRC, shirika la OCHA kusema kuongezeka kwa mapigano huko Kivu Kaskazini kumesababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao.

    Nchi ya Chad, ina rais mpya ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno, kadhalika tutaangazia hali kule Gaza na nchini Ukraine.

    Sat, 11 May 2024
  • 291 - Athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki haswa nchini Kenya

    Wiki hii baadhi ya mambo tunayoangazia ni athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki, pia mgogoro kule Sudan, lakini pia kauli ya Ufaransa kwa Rwanda kuacha kuunga mkono kundi la M23 kule DRC. Kadhalika tutaangazia uhuru wa vyombo vya habari kuminywa nchini Burkina Faso lakini pia kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

    Sat, 04 May 2024
  • 290 - Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika ,mafuriko yaripotiwa Kenya

    Makala haya yanaangazia yaliyojiri nchini Kenya na Tanzania kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 ,mgomo wa madaktari nchini Kenya, Tanzania kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, safari za wahamiaji walioko nchini Uingereza kuelekea nchini Rwanda

    Tutaangazia pia uchaguzi wa wabunge nchini Togo,usalama wa Burkina Faso , na Ulimweguni  tutazidi kuangazia Mzozo unaondelea baina ya Israel na Hamas .

    Sat, 27 Apr 2024
  • 289 - Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC

    Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.

    Sat, 20 Apr 2024
Mostra altri episodi