Nach Genre filtern
- 11648 - Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"Thu, 02 May 2024
- 11647 - 02 MEI 2024
- Nchini Kenya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameathiri maelfu ya watu yakisababisha vifo na kuwaacha wengi bila makazi. Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirikaRipoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi ESCWA inasema vita inayoendelea Gaza imesababisha athari mbaya za kiuchumi na maendeleo ya binadamu katika eneo zima la Palestina.Niger mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 na ongezeko hili na wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno ELEKEZA NA ELEZA!
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 02 May 2024 - 11646 - Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi. Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).
Wed, 01 May 2024 - 11645 - UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP ambapo kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana”
Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi, na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "
Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia mashambulizi yanayoendelea likisema“kumekuwa na zaidi ya mashambulizi 360 kwenye vituo vyake tangu kuanza kwa vita. Mbali na makumi ya maelfu ya waathiriwa, miundombinu muhimu imeathiriwa pia, pamoja na kisima cha maji cha shirika hilo kilichoko katika jiji la Khan Younis.”
Na ili kukarabati chanzo hicho cha maji UNRWA inasema kunahitajika kuondoa tani za uchafu ikiwemo vilipuzi na vifaa vingie vya mabaki ya virta kama vilivyobainiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada wa kutegua mabomu UNMAS nav yote vinahitaji kuondolewa kwa usalama kipande kwa kipande,."
Na wizara ya afya ya Gaza imeonya kwamba endapo hakutopatikana usitishwaji mapigano basi Maisha ya watu yataendelea kukatiliwa zaidi na hali itakuwa janga kubwa la kibinadamu kwani hadi sasa takriban watu 34,568 wameuawa na 77,765 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7 mwaka jana.
Wed, 01 May 2024 - 11644 - 01 MEI 2024
- Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, ambapo mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Makala inaangazia changamoto za mabadiliko ya tabianchi zilizowalazimisha wanawake wa jamii ya Kimaasai nchini Kenya kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na athari hizo ili kujikimu kimaisha.Na katika mashinani inayotupeleka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Goma Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo vurugu za kutumia silaha zinaendelea kusababisha raia kupoteza maisha yao. Katika video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi DRC, wanawake wanaomba amani irejee.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wed, 01 May 2024 - 11643 - UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka
Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.
Ninapoona plastiki naona fursa za ajira! Ni kauli hiyo ya Raphael Bassemi, mkimbizi kutoka DRC akiwa hapa kambini Kakuma akizungumza huku wanawake na wanaume waliovalia maovaroli na glovu na barakoa wakiokota taka. Anasema anafurahi anapoona jamii inashiriki na zaidi ya yote wanawake wasiokuwa na ajira sasa wameajiriwa, "Nilipoanza nilijikita tu kwenye plastiki, lakini ilibainika kuwa kuna takangumu nyingi za kudhibitiwa. Sasa ninajishughulisha na aina zote za taka.”
Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaonesha taka mbalimbali zikiwemo mifupa ya mafuvu ya ng’ombe, vyuma, seng’eng’e na kadhalika. Sasa amesharejeleza tani zipatazo 100 za takangumu.
"Tunatengeneza rula kwa ajili ya wanafunzi, vibanio vya kuanikia nguo, sahani za kulia chakula na vikombe vya chai na kahawa. »
Raphael na wenzake wakiwa kwenye kiwanda hiki alichoanzisha wanapata ugeni ukiongozwa na Dominique Hyde kutoka UNCHR. Baada ya ziara, Bi. Hyde anasema, "Kilichotuvutia ni jinsi wanaweka mawazo yao kwenye hii biashara ili istawi, na pia kushirikisha jamii ipate ajira na hatimaye kipato walipie elimu na umeme. Kama sisi sote tunahitaji kazi, wao wanahitaji kazi, na wao wameanzisha hii ajira wenyewe. »
Sasa Raphael anasema jamii ina furaha naye ana furaha na zaidi ya yote.
"Ninapoona wanawake ninaofanya nao kazi wana furaha, nami nina furaha na ninatamani kuchukua hatua zaidi."
Wed, 01 May 2024 - 11642 - Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki ambao walikuja katika jukwaaa hilo na azimio maalum linalohimiza mama kuvaa kofia yake ili kusaidia kutatua migogoro kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi kimataifa. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili akianza kwa kufafanua kuhusu azimio hilo
Tue, 30 Apr 2024 - 11641 - 30 APRIL 2024
- Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4. Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,"Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linashirikisha wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira kupitia upandaji miti na kupitia video iliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus FM nampisha mwanaharakati wa mazingira ambaye alitembelea eneo Bunge la Ngong katika kaunti ya Kajiado jijini Nairobi ili kushirikiana na wanafunzi katika kutimiza wito wa UNEP wa upanzi wa miti.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 30 Apr 2024 - 11640 - Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund
Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.
Mon, 29 Apr 2024 - 11639 - 29 APRILI 2024
- Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi. Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.Mashinani ikiwa ni wiki ya chanjo, kniniki tembezi inayofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imekuwa uti wa mgongo wa mfumo wa afya nchini Somalia na tunakutana na Jamila Moham, Mhudumu wa afya ya jamii katika kijiji cha Dhusamareeb.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Mon, 29 Apr 2024 - 11638 - UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza
Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.
Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.
Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.
UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.
Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhimu kama maji ya kunywa ambapo wakimbizi wa ndani wanapokea chini ya lita moja ya maji kwa mtu kwa ajili ya kunywa, kufua na kuonga ikiwa ni tofauto kubwa na lita 151 ambacho ni kiwango cha chini wanachostahili kupata.
Na jana Jumapili UNRWA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada w uteguzi wa mabomu UNMAS walianza operesheni muhimu ya kutathimini uharibifu katika vituo vya UNRWA kuweka alama kwa makombora yoyote na vifaa vyovyote ambavyo hvijalipuka.
Mitambo 165 ya UNRWA huko Ukanda wa Gaza imeathiriwa wakati wa vita hii inayoendelea.
Na UNMAS inasema ili kuifanya Gaza kuwa salama dhidi ya vifaa vya milipuko ambayo haijalipuka inaweza kuchukua miaka 14.
Mon, 29 Apr 2024 - 11637 - Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji
Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi
Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii.
Mbinu hii inayoendeshwa na wana jumuiya wenyewe inaweka kiwango kipya cha usaidizi wa kibinadamu nchini humo, kama anavyoeleza Mola Suleiman ambaye ni Mshiriki wa Msaada wa WFP anasema, "Wanaotambua wenye uhitaji zaidi sio viongozi, bali watu wasioegemea upande wowote waliochaguliwa na jamii. Tunaweza kwenda kwenye madawati ya usaidizi yaliyoanzishwa huko wilayani Kebeles na viunga vyake na kupeleka malalamiko yetu. Kwa kufuata utaratibu wa uwazi, tunakagua na kuthibitisha wale waliochaguliwa na jumuiya pana, kwakweli huu mfumo ni bora kuliko ule wa awali”
Selam Ambachew ni mwanakamati aliyechaguliwa na jamii.
"Kama jumuiya, tulichagua kamati, kisha kamati ikaanza tathmini yake, tunapokea orodha ya watu wote wanaoishi katika eneo hili, na tunachunguza orodha ili kuona ni nani anayefaa kwa vigezo vya usaidizi katika jamii"
Tadel Gebeyehu ni mmoja wa wananchi walionufaika na mfumo huu mpya wa jamii yenyewe kuchagua wenye uhitaji zaidi wa Msaada wa kibinadamu, anasema "Tulipewa kadi za mgao na lazima tuzioneshe tunapokwenda kupokea chakula. Kadi hizi za mgawo ni muhimu kwa sababu zinazuia watu masikini kunyanyaswa"
Ama hakika mwitikio wa kibinadamu nchini Ethiopia unazingatia uwazi, unaendeshwa kwa kuzingatia takwimu na kufikia wale wenye uhitaji zaidi, na hili linathibitishwa Haftom Gebretsadik mmoja wa wagawaji wa msaada.
“Mchakato wa kugawa Msaada ni mzuri sana, kila nyanja ni nzuri sana, kinachofanya uwe ya kipekee ni heshima ya utu na ubinadamu. Mfumo ni wa uwazi, hakuna mkanganyiko wala wizi, kwa ujumla mchakato huo ni wa kupongezwa”.
Mon, 29 Apr 2024 - 11636 - Mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika migogoro katika jamii za asili - Alois Porokwa
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili iliyopita lilipewa kipaumbele cha juu wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 jijini Nairobi, Kenya. Wakati huo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.
Fri, 26 Apr 2024 - 11635 - Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.
Fri, 26 Apr 2024 - 11634 - 26 APRILI 2024
- Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.Na tukisalia nchini Sudan, mwaka mmoja wa mzozo umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Katika makala Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanahaha kushughulikia changamoto za usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Fri, 26 Apr 2024 - 11633 - Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan
Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito.
Fatima sio jina lake halisi, tunalitumia hili ili kuficha utambulisho wake na hapa anaanza kueleza yale yaliyomsibu akiwa mikononi mwa wanamgambo wenye silaha.
“Nilibakwa mara tatu. Aliniambia lala chini, usipotaka kulala chini naweza kukuuwa. Sijui sasa kama ni huyo mwanaume aliniingilia mara tatu au kulikuwa na wengine.”
Akiwa na kiwewe na aliyekata tamaa, Fatima akaukimbia mji wake wa Khartoum akiwa na watoto wake kwenda kusini mashariki mwa Sudan, kusaka hifadhi na alipofika huko, anasema “Nilikwenda kuripoti tukio hilo katika kliniki na kusaka msaada ili waweze kunifanyia uchunguzi wa jumla. Nikaenda hospitalini na kila kitu kilikuwa sawa. Baada ya miezi miwili nilienda tena kliniki na wafagundua kuwa nina ujauzito.”
Pole sana Fatima, sasa ni nini unachohitaji wakati huu nchi yako bado ingali vitani?
“Tunahitaji amani kwa ajili yetu, ili tuweze kurudi na kuishi nchini Sudan.”
Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama vile UN WOMEN, OCHA, UNHCR na hata Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili wa Kingono kwenye mizozo wamekuwa wakipazia unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudan huku wakieleza wasiwasi wao mkubwa kuwa ukubwa halisi wa mgogoro bado haujajulikana na kumekuwa na viwango vidogo vya kuripoti matukio ya kikatili kwani baadhi ya wanawake na wasichana wanaogopa unyanyapaa na kutokuwa na imani na taasisi za kitaifa.
Fri, 26 Apr 2024 - 11632 - Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.
Thu, 25 Apr 2024 - 11631 - Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”Thu, 25 Apr 2024
- 11630 - 25 APRILI 2024
- Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo mwaka huu inahamasisha kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huu ili kuwa na ulimwengu wenye usawa zaidi kwani imebainika kuwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ndio wanaoathirika zaidi.Leo pia ni siku ya kimataifa ya wasichana katika tehama na mwaka huu inasherehekea uongozi ikisisitiza hitaji muhimu la kuwa na mifano thabiti ya wanawake viongozi katika taaluma ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati -STEM kwani hali ilivyo sasa kuna wanawake viongozi wachache katika maeneo hayo. Na tukisalia na masuala ya wasichana katika tehama Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa ripoti inayoonya kuwa pamoja na faida za kufundisha na kujifunza kidigitali maendeleo hayo ya kidigitali yanaweza kuwaathiri wasichana kwa kuingilia faragha zao, kuvuruga masomo yao na unyanyasaji mtandaoni.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Thu, 25 Apr 2024 - 11629 - Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto. Prisca na wenzake kutokana na kupenda kazi yao wanafanya kila njia iwe ni kutumia usafiri wa bodaboda au hata kuvuka mito na mabonde kwa miguu kuhakikisha chanjo zinafika. Kufahamu kwa kina ungana na Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Tanzania.
Wed, 24 Apr 2024 - 11628 - Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.
(Taarifa ya Anold Kayanda)
Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.
Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.
WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.
Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani.
WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo.
Tags: Siku za UN, WHO, Chanjo, EPI, Wiki ya Chanjo Duniani
Wed, 24 Apr 2024 - 11627 - Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO
Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023.
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Asante Leah. Kwa hakika ripoti hiyo ya “Mgogoro wa kimataifa wa chakula” GRFC inasema kiwango cha watu wenye njaa duniani kiliongezeka kwa watu milioni 24 kutoka mwaka 2022 hadi 2023 na ni asilimia 21.5 ya watu waliofanyiwa tahimini na hicho ni kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19 limesema shirika la FAO likiongeza kuwa idadi ya walio na njaa duniani inaendelea kuongezeka.
Ripoti imetaja sababu kuu tatu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa janga la njaa duniani ambazo ni mosi migogoro na vita ambapo inasema inaathiri katika nchi 20 zilizo na jumla ya watu milioni 135 wanaokabiliwa na njaa zikiwemo Sudan, Yemen na Palestina katika Ukanda wa Gaza.
Pili ni matukio mabaya ya hali ya hewa yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa chanzo cha njaa katika nchi 18 na kuathiri kwa njaa zaidi ya watu milioni 77.
Na tatu mdororo wa kiuchumi uliokuwa chachu ya njaa katika nchi 21 na kuathiri jumlaya watu milioni 75.
FAO imesema kwa miaka minne mfululizo takriban asilimia 22 ya watu waliofanyiwa tathimini duniani wamekuwa wakikabiliwa na kutakuwa na uhakika wa chakula. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Mgogoro huu unahitaji hatua za haraka. Kutumia takwimu zilizoainishwa katika ripoti hii ili kufanyia marekebisho mifumo ya chakula na kushughulikia mizizi ya kutakuwa na uhakika wa chakula itakuwa muhimu sana”
Kwa mujibu wa ripoti waathirika wakubwa ni watoto, wanawake na watu wenye ulemavu.Mtandao wa kimataifa dhidi ya mgogoro wa chakula imetoa wito wa haraka wa kubadili mtazamo ili ujumuishe amani, hatua za kuzuia na za maendeleo sambaba na juhudi za dharura kuvunja mzunguko wa janga la njaa ambalo linasalia katika viwango vya juu
Wed, 24 Apr 2024 - 11626 - 24 APRILI 2024Wed, 24 Apr 2024
- 11625 - 23 APRILI 2024
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP.
Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na kuongezeka kwa mlipuko wa ugonjwa wakipindi pindu duniani.
Kwa upande wa mashinani hii leo utasikia kuhusu harakati za mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha usalama wa mipaka.
Tue, 23 Apr 2024 - 11624 - Rein Paulsen: Wakati wa kuchukua hatua kuepusha baa la njaa Sudan ni sasa
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Sabrina Moshi anasimulia.
Mon, 22 Apr 2024 - 11623 - DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani
Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao.
Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu.
“Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzitumia vyema na kuzisambaza, lakini sio jambo la maana kwani kitendo hicho ni kusema tuna sawazisha hali mbaya zaidi ya Kivu Kaskazini ni kwamba tunapaswa kupungua, inaweza kuwa ituri au Kivu Kusini. Hayo pia ni maamuzi magumu kwa sababu kuna watu wengi ambao hawana uhakika wa chakula katika maeneo hayo pia.”
Bi.Jones amesema pamoja na kuwa na fahari na kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia wakimbizi wengi hapo awali, mtiririko mkubwa wa wakimbizi wanaowasili kusaka hifadhi katika makambi katika miezi ya hivi karibuni umefanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.
Mon, 22 Apr 2024 - 11622 - 22 APRILI 2024
- Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa.Na mashinani tutapeleka Tambunra nchini Sudan Kusini kumsikia mkimbizi wa ndani akisihi kurejea kwa amani illi aweze kurudia nyumbani.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 22 Apr 2024 - 11621 - ILO: Joto la kupindukia linaathiri asilimia 70 yawafanyakazi kote duniani
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Asante Anold, akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Manal Azzi, afisa wa masuala ya usalama kazini na afya wa shirika la ILO amesema takwimu hizi za kustaajabisha zinasisitiza haja kubwa ya kurekebisha hatua zilizopo za usalama na afya kazini ili kushughulikia ipasavyo vitisho vinayojitokeza kutokana na hatari zinazohusiana na changamoto za hali ya hewa.
Ameongeza kuwa “Zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wetu wanakabiliwa na joto jingi, angalau joto la kupindukia, katika wakati mmoja wa maisha yao ya kazi. Hiyo ni jumla ya wafanyakazi bilioni 2.4 duniani kote, kati ya wafanyakazi wa kimataifa wa bilioni 3.4.”
Ripoti hiyo iliyopewa jina “Kuhakikisha usalama na afya kazini katika mazingira yanayobadilika” inaeleza kwamba mabadiliko ya tabianchi tayari yameleta athari kubwa kwa usalama na afya ya wafanyakazi katika kanda zote duniani.
Kwa mujibu wa ILO waafanyakazi, hasa wale walio katika maeneo yenye umaskini zaidi duniani, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi kama vile joto kali, ukame wa muda mrefu, moto mkubwa wa nyika, na vimbunga vikali.
Bi. Azzi amesema "Wafanyakazi zaidi ya milioni 22 wanaugua magonjwa na majeraha yanayohusiana na joto kali na haya yanaweza kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ajali katika usafiri, katika ajali za barabarani kutokana na usingizi kwa kutolala vizuri usiku kwa sababu kulikuwa na joto kupita kiasi, hadi ajali za ujenzi, majeraha, kuteleza na kuanguka. kunkohusiana na ongezeko la joto kali."
Ripoti hiyo inabainisha kuwa baadhi ya athari za kiafya kwa wafanyakazi zilizohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, ni pamoja na saratani, ugonjwa wa moyo na mishipa, magonjwa ya kupumua, figo kuharibika na hali ya afya ya akili.
Pia kuongezeka kwa joto na unyevu wa hali ya juu, dawa nyingi za wadudu hutumiwa katika sekta ya kilimo na kufanya wafanyikazi milioni 870 katika kilimo kuwa na uwezekano wa kuathiriwa na viuatilifu, huku kukiwa na zaidi ya vifo 300,000 vinavyohusishwa na sumu ya dawa hizo kila mwaka.
Bi Azzi amesisitiza kuwa mambo haya yote yanaingiliana na kwamba zana zinazofaa zinapaswa kuwepo ili kupima athari na kuwa na uwezo wa kufanyia kazi mapendekezo.
Mkutano mkuu umepangwa kufanyika 2025 na ILO kwa kushirikisha wawakilishi wa serikali, waajiri na wafanyakazi ili kutoa mwongozo wa sera kuhusu hatari za mabadiliko ya tabianchi katika masuala ya kazi.
Mon, 22 Apr 2024 - 11620 - Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT
Lugha ni miongoni mwa njia za kimsingi za kujenga utangamano duniani. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa lugha ni chombo cha kusongesha tamaduni na miongoni mwa lugha zilizotengewa siku mahsusi kusherehekewa ni kichina ambacho shamrashamra zake ni tarehe20 mwezi Aprili ya kila mwaka.Lugha hii imesambaa duniani ikiwemo Tanzania ambako hii leo Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki amefuatilia mafunzo yake kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.
Sat, 20 Apr 2024 - 11619 - Joram Nkumbi na Vivian Joseph: Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza toka kwa wenzetuFri, 19 Apr 2024
- 11618 - Francesco La Camera: Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kuhamia haraka katika nishati jadidifuFri, 19 Apr 2024
- 11617 - 19 APRILI 2024
Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.
Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.
Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.
Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Fri, 19 Apr 2024 - 11616 - Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhiri na hadhiri.”Thu, 18 Apr 2024
- 11615 - 18 APRILI 2024
- Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023. Mkutano wa Wiki ya Uendelevu ya Umoja wa Mataifa unaendelea hapa Makao Makuu New York Marekani, leo ukijikita na mada ya miundombinu endelevu na inayoaminika ambayo Umoja wa Mataifa unasema itazisaidia nchi kuelekea kwenye maendeleo yenye miumbombinu bora, isiyo ya hatari na itakayoongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na hadhiri.”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 18 Apr 2024 - 11614 - Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..
Wed, 17 Apr 2024 - 11613 - Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.
Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.
Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi jimboni Ituri. Taswira ya angani kutoka ndege hii ya Umoja wa Mataifa na kisha wanawasili. Mapokezi hapa Bunia, kutoka kwa wenyeji wao.
Moja kwa moja msafara wao wa magari unafika kwenye kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji wa Bunia na wanaingia ndani ambako wanawake, wanaume na watoto, wazee na vijana, nyuso zao zinaonesha matuamini kwani wahenga walinena mgeni njoo mwenyeji apone.
Mkalimani akamweleza Turk kuwa wanachosema maeneo yao yametawaliwa na waasi na hawawezi kurejea makwao.
Na ndipo Kamishna huyu Mkuu wa Haki za Binadamu baada ya kuwasikiliza wakimbizi na kuzungumza nao akatoka nje na kusema, “Nimekutana na kundi la watu ambao wamefurushwa makwao kutokana na mauaji ya kikatili na ya kutisha yaliyotekelezwa kwenye makazi yao. Na wamekuweko hapa kwa miaka minne sasa. Tamanio lao kubwa kabisa ni kuweza kurejea makwao.”
Kwa sasa kuna takribani watu milioni 1.8 waliofurushwa makwao jimboni Ituri kati ya wakimbizi wote wa ndani milioni 7.2 nchini kote DRC.
Kesho Bwana Turk atakuwa na mazungumzo na Rais President Félix Tshisekedi na maafisa wengine wa serikali, Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na vyama vya siasa pamoja na watetezi wa haki za binadamu na kisha atazungumza na waandishi wa habari.
Wed, 17 Apr 2024 - 11612 - 17 APRILI 2024
- Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukkwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania.Na mashinani tutakupeleka nchini Madagascar kusikia ujumbe kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini kwanza ni makala.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Wed, 17 Apr 2024 - 11611 - Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia
Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.
Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu.
Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.
Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati wa msimu wa muwambo kati ya mwezi Julai na Septemba.
Viwango vya utapiamlo katika sehemu za Afar, Amhara, Tigray na mikoa mingine vinatia wasiwasi mkubwa na vinaendelea kuwa vibaya zaidi. Wakati huo huo, migogoro katika Tigray na mikoa mingine imeharibu maelfu ya shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya jamii.
Mama huyu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni wa eneo la Afar, mashariki mwa Ethiopia ambako pia kumeathiriwa na mafuriko anapaza sauti akisema, “Ninataka kulea na kusomesha watoto wangu vizuri. Nawatakia watoto wangu mema.”
Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wanaunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kuongeza msaada wa kuokoa maisha kwa watu milioni 15.5, na msaada wa chakula kwa watu milioni 10.4 nchini humo Ethiopia. Kwa mwaka mzima, ili mpango huo ufanikiwe unahitaji dola za Marekani bilioni 3.24.
Wed, 17 Apr 2024 - 11610 - 16 APRILI 2024
- Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 ya kibinadamu, ya maendeleo na serikali wametoa ombi la haraka la dola milioni 112 ili kuwasaidia zaidi ya wahamiaji milioni 2.1 na jamii zinazowahifadhi. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na jamii hizo ni katika njia za uhamiaji za Mashariki na Kusini zkijumuisha Djibouti, Ethiopia, Somalia, Yemen, Kenya na Tanzania.Na mashinani leo tunakwenda mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususan jimboni Ituri ambako huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umechukua hatua kukabili mashambulizi kutoka waasi, mashambulizi ambayo kila uchao yanazidi kufurusha raia. Mzungumzaji wetu ni Luteni Kanali Mensah Kedagni, msemaji wa kijeshi wa MONUSCO.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 16 Apr 2024 - 11609 - Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa
Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.
Mon, 15 Apr 2024 - 11608 - Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali.
Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis.
Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili.
Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili.
Mwenyekiti wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusuu watu wa asili Bi. Hindou Oumarou Ibrahim akizungumza katika jukwaa hilo amesema “Kuondolewa vikwazo kwenye upatikanaji wa fedha ni muhimu ili kuhakikisha watu wa asili wanatekeleza kwa vitendo mipango yao na kuwa na njia ya kudumisha kujitawala,”
Kwa upande wake Bwana Li Junhua, ambaye ni msaidizi waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) amesema “unahitaji ufadhili wa muda mrefu, unaotabirika, na wa moja kwa moja kwa Watu wa Asili, ikijumuisha kupitia mifumo ya ufadhili ya umma, ya kibinafsi, na inayoongozwa na Wenyeji ambayo inashirikisha kikamilifu Wanawake na vijana wa kiasili.”
Unaweza kufuatilia moja kwa moja matangazo ya jukwaa hili yanayorushwa mubashara na Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake wa UN Web TV,matangazo yanarushwa kwa lugha rasmi sita za umoja wa Mataifa ambazo ni Kingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.
Mon, 15 Apr 2024 - 11607 - 15 APRILI 2024
- Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Makala Stella Vuzo, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, anatuletea mazungumzo kati yake na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhudhuria wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika mwezi uliopita jijini Nairobi, Kenya. Kwa kuwa jamii zinazoishi kiasili wakati mwingine zimekuwa zikilaumiwa kuwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.Na mashinani tunamulika vita nchini Sudan ambayo inaendelea kuwalazimisha mamilioni ya watu kukimbia kuokoa maisha yao. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mkimbizi ambaye alikimbia machafuko nchini humo kuelekea Chad anasimulia changamoto alizozipitia.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mon, 15 Apr 2024 - 11606 - UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi
Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.
Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa.
Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiingereza, inaonesha ukweli mchungu wa kufanikisha safari hiyo kwa mtoto nchini Nigeria kuweko shuleni bila uoga.
Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Cristian Munduate amesema tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok ni kengela ya kutuamsha juu ya hatari kubwa watoto wetu wanakabiliwa nayo wanaposaka elimu.
Anasema leo tunapotafakari janga hili na mengine ya hivi karibuni ni dhahiri kuwa juhudi zetu za kulinda mustakabali wa watoto wetu lazima ziimarishwe.
Mwakilishi huyo anasema kwa kuzingatia takwimu zilizotolewa na ambazo zinatia hofu kubwa, ni lazima kupata majawabu ya sio tu dalili bali pia chanzo cha janga hilo la utekaji nyara watoto.
Bi. Munduate amekumbusha kuwa elimu ni haki ya msingi na ni njia muhimu ya kuelekea kuondokana na umaskini. Lakini kwa watoto wengi nchini Nigeria inasalia kuwa ndoto isiyotimizika.
Ripoti ilimulika maeneo 6 ikiwemo mifumo thabiti ya shule, ukatili dhidi ya watoto, majanga ya asili,mizozo ya kila siku na miunmdombinu ya shule na kubaini utofauti mkubwa wa vigezo hivyo katika majimbo yote 36.
Jimbo la Borno liko thabiti kwani limekidhi viwango kwa asilimia 70 ilhali majimbo ya Kaduna na Sokoto bado yako nyuma.
Uchambuzi huu unakuja wakati kuna ripoti za ongezeko la ghasia dhidi ya shule ambapo katika miaka 10 iliyopita, matukio ya mashambulizi yamesababisha watoto zaidi ya 1,680 kutekwa nyara wakiwa shuleni au kwinigneko.
UNICEF inataka Nigeria pamoja na mambo mengine ihakikishe shule kwenye majimbo yote zina rasilimali za kutekeleza MSSS.
Pia itatue pengo la uwiano wa usawa katika hatua za kuimarisha usalama shuleni. Nigeria pia iimarishe usimamizi wa sheria na mikakati ya usalama ya kulinda taasisi za elimu na jamii dhidi ya utekwaji.
Kwa sasa UNICEF inashirikiana na serikali kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mazingira salama ya kusomea.
Soma ripoti nzima hapa.
Mon, 15 Apr 2024 - 11605 - Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona.
Tukio lilianza kwa ukumbi kuwa giza na video ya dakika tano ikachezwa kueleza kuwa watu wengi wanaijua Rwanda kuanzia 1994, lakini ilikuweko hata kabla ya ukoloni, na kwamba wakoloni ndio waligawa watu kwa misingi ya makundi licha ya kwamba lugha yao ilikuwa moja. Manusura na watekelezaji wa mauaji walizungumza pia kwenye video hiyo!
Video ikafuatiwa na kuwasha mishumaa kukumbuka waliouawa na kisha hotuba ambapo Katibu Mkuu Guterres akawa ana ujumbe mahsusi kwa vijana wa Rwanda walioshiriki kimtandao na pia ukumbini.
Anasema rafiki zangu, katu hatutasahau vitisho vya siku 100. Lakini tunahitaji msaada wenu. Tunahitaij sauti na uchechemuzi wenu kusongesha kumbukizi za wale waliouawa. Na kukemea chuki kokote muisikiako au muionapo. Mijini kwenu, vitongojini, shuleni, mtandaoni, popote pale na kila mahali.
Akaendelea kusema kuwa hebu na tuondoe chuki na ukosefu wa stahmala kokote tuvionapo. Kumbukumbu za waliouawa zichochee vitendo vyetu, na azma yetu ya kuhakikisha dunia bora na salama kwa watu wote.
Guterres amesema Umoja wa Mataifa kila wakati utashikamana na vijana katika juhudi hizo muhimu.
Mauaji ya kimbari Rwanda ya mwaka 1994 yalifanyika kwa siku 100 kuanzia tarehe 7 Aprili na zaidi ya watu milioni moja waliuawa, wengi wao Watutsi, halikadhalika wahutu wenye msimamo wa kati na watu wengine waliokuwa wanapinga mauaji hayo.
Katibu Mkuu amesema siku hizo 100 ziliakisi ubaya zaidi wa ubinadamu. Lakini kipindi baada ya mauaji kilidhihirisha ubora wa roho ya ubinadamu: mnepo, maridhiano, ujasiri na nguvu.
Amesema simulizi za manusura ni ushahidi wa nguvu ya matumaini na msamaha ambapo amemtaja manusura Laurence Niyonangira ambaye alipoteza jamaa zake 37 wakati wa mauaji hayo.
“Alichagua kusamehe mmoja wa wahusika wa mauaji ya familia yake baada ya mhusika kuungama na kutumikia muda jela kwa makosa aliyotenda. Kama manusura, Laurence alisema ‘tunaweza kuponya vidonda kwa kushirikiana wale waliovisababisha.” Amesema Guterres.
Hivyo Katibu Mkuu amesema mwaka huu ambapo kumbukizi inajikita kwenye mzizi wa mauaji ya kimbari ambao ni chuki, ambayo sasa inakolezwa na mitandao ya kijamii, “ni lazima tushikamane pamoja na kurejelea shinikizo la dunia la kuridhia na kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya kimbari, huku tukiimarisha mifumo ya kuzuia, kuelimisha vizazi vipya kuhusu mauaji ya kimbari yaliyopita na kukabili taarifa potofu na za uongo ambazo huchochea kauli za chuki na nia na vitendo ya mauaji ya kimbari.”
Fri, 12 Apr 2024 - 11604 - Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC
Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu ni Kapteni Fadhila Nayopa, Afisa habari wa kikosi hicho.
Fri, 12 Apr 2024 - 11603 - 12 APRILI 2024
- Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona.Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.Na mashinani tunakuletea ujumbe wa Marthe Nyangoma, mtumishi wa umma kutoka eneo la Irumu, huko Ituri nchini DRC, ambaye kwa uwezeshaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, anahamasisha jamii dhidi ya taarifa potofu na kauli za chuki akisistiza kuwa kabla ya kuwasilisha taarifa, lazima zidhibitishwe ili kuepusha mgawanyiko.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Fri, 12 Apr 2024 - 11602 - Wakimbizi kutoka Sudan wanoingia Sudan Kusini wanaendelea kuongezeka
Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.
Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP inaanza kwa kuonesha wananchi wakiwa na vifurushi mikononi, wengine wakiwa wamepanda usafiri unaosukumwa na ngombe na wengine mabasi wakiingia katika mpaka wa Joda nchini Sudan kusini wakitokea nchini Sudan.
“Tumesafiri kwakutumia basi na imetuchukua siku mbili kufika hapa”, ndivyo anavyosema Hamida Ibrahim mkimbizi kutoka Sudan. Anaendelea kwa kueleza kile wanachohitaji kwa sasa.
“Tunahitaji chakula. Huo ndio msaada wa haraka tunaohitaji ili tuweze kuishi. Kwa sababu tupo na watoto na hawana uwoga wanachojua wanakuja hapa kufata usalama”
Kiongozi wa WFP katika eneo hili Leonidace Rugemalila anasema mzozo huu wa Sudan umemuathiri kila mtu.
“Katika kipindi cha miezi mitatu idadi ya watu wanaovuka mpaka huu kila siku imeongezeka kutoka watu 1,500 mpaka takriban watu 2,500.”
Naye Mkuu wa lishe Aachal Chand anasema wengi wa waaathirika wa mzozo nchini Sudan ni wanawake na watoto, na walioathirika zaidi ni wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Wanapovuka mpaka, mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka mitano anapatiwa biskuti za lishe kama chakula cha haraka chakumpa lishe. Kwa watoto chini ya miaka mitano tunawapa chakula maalum cha lishe. Kuanzia saa mbili asubuhi mpaka wakati huu saa 10 jioni wameshatoa lishe kwa takriban watoto 400 ambao wamepokea matibabu ya utapiamlo au huduma za matibabu.”
Chand ameeleza kuwa WFP na wadau wake wanaendelea kutoa msaada hata hivyo wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.
“Watu wanahitaji msaada wa afya na lishe, watu wanahitaji usaidizi katika kupata uhakika wa chakula, watu wanahitaji msaada wa kuweza kuwasaidia kufika katika maeneo wanayotaka kuelekea.Sudan na athari zake kwa nchini ya Sudan Kusini zinasahaulika na tunatakiwa kuhakikisha hatusahau mzozo huu kwasababu hawa ni watu na wanapata athari halisi katika maisha yao.”
Fri, 12 Apr 2024 - 11601 - 11 APRILI 2024
- Wakati mgogoro nchini Sudan ukiingia katika mwaka wake wa pili, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kutafuta Ukweli nchini Sudan umezitaka pande zinazokinzana zisitishe mapigano, zilinde raia na kuruhusu mtiririko wa misaada. Taarifa iliyochapishwa leo na OHCHR imemnukuu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Mohamed Chande Othman akisema, "Pande zinazopigana Sudan zina wajibu wa kisheria kuwalinda raia, lakini zimeonesha kutojali kufanya hivyo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetangaza kwamba moja ya magari yake jana yakisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza lilishambuliwa kwa risasi za moto. Pia UNICEF imechapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X video ya Msemaji wa shirika hilo, Tess Ingram akiwa katika hospitali ya Deir Al Balah, akizungumza kuhusu mtoto Omar mwenye umri wa miaka saba ambaye amelazwa hapo akisumbuliwa na utapiamlo baada ya kula nyasi kwa wiki kadhaa zilizopita. Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limezindua mradi wa thamani ya euro milioni 15 sawa na dola milioni 16.29 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya (EU) ili kusaidia sekta ya misitu ya Uganda kuchangia kwa uendelevu zaidi kwa uchumi na mazingira. Mpango wa miaka mitano wa Minyororo ya Thamani Endelevu ya malighafi za miti nchini Uganda, unalenga kuhakikisha upatikanaji endelevu wa malighafi halali za miti kutoka katika misitu iliyopandwa, kuongeza uwezo wa usindikaji na mahitaji ya soko ya bidhaa za mbao na kuboresha uwepo na upatikanaji wa ufadhili nafuu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 11 Apr 2024 - 11600 - Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”Thu, 11 Apr 2024
- 11599 - Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi
Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani. Manusura wa mauaji hayo wanasemaje kuhusu kumbukumbu hii? Na je dunia imejifunza nini kutokana na mauaji hayo ya Rwanda taifa ambalo limeshafungua ukurasa mpya na kuyapa kisogo? Twende mjini Kigali ambako kumbukumbu kubwa imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100, shuhuda wetu ni Eugene Uwimana afisa mawasiliano wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.
Tue, 09 Apr 2024 - 11598 - 09 APRILI 2024
- Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Olga Sarrado Mur katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza kwamba vita nchini Sudan ikikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili na ikiendelea kupamba moto, idadi ya Wasudan waliolazimika kukimbia sasa imepita watu milioni 8.5, huku milioni 1.8 kati yao wakiwa wamevuka mipaka ya nchi. Na kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo, idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na virusi vya homa ya ini inaongezeka. Ugonjwa huo ni wa pili kwa kusababisha vifo vya watu milioni 1.3 kwa mwaka, sawa na ugonjwa wa kifua kikuu, ambao ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababisha vifo vingi zaidi kwa sasa. Hata hivyo WHO inasema lengo la kutokomeza Homa ya ini ifikapo 2030 bado linapaswa kufikiwa.Na katika mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ujumbe kuhusu hatari vilipuzi na mabomu ya kutegwa ardhini, salia hapo tafadhali.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 09 Apr 2024 - 11597 - Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo.
“Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma”
Kwa Mariam matunda ya kazi yake yako dhahiri.
“Moja ya kazi zangu zinazovutia ambazo nimefanya ni lango kuu la kliniki 4”
Pamoja na mafanikio hayo Marian anatamani kusoma zaidi kuongeza ujuzi.
“Nilisoma hadi daraja la sita hiyo ni ngazi ya Diploma. Natamani kuchimba ndani zaidi ya hii tasnia ya kuchomelea vyuma lakini hapa Kenya hatuna hiyo kozi. Ipo katika taasisi ya uchomeleaji vyuma ya Afrika Kusini. Ningependa kwenda huko na kusoma uchomeleaji vyuma chini ya maji.”
Na kwa kuwa yeye ameweza anaamini hakuna kinachomshinda mwanamke kwani
“Wanawake tuna uwezo, wanawake tuna ujuzi, wanawake tunaweza kufanyakazi zinazofanywa na wanaume, wanawake tunaweza kufurahia kazi zetu, wanawake hebu tusimame kidete tunaweza”
Mon, 08 Apr 2024 - 11596 - Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO
Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.
Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.
Mon, 08 Apr 2024 - 11595 - 08 APRILI 2024
- Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Katika makala makala ambapo Assumpta Massoi anatupeleka jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia manufaa ya uwepo wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO ambao sasa unafunga virago baada ya kuhudumu kwa miaka 22.Na katika mashinani tutakuwa Tanzania kuangalia endapo lengo la ujumuishwaji wanawake katika huduma za kifedha litatimia ifikapo mwaka 2030.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 08 Apr 2024 - 11594 - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili ombi la Palestina kuwa mwanachama
Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ratiba ya mikutano hii leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa Baraza la Usalama lenye wajumbe 15 kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa sita kamili mchana kwa saa za New York Marekani, litakutana kwanza katika kikao cha faragha na kisha kikao kitafunguliwa kwa umma kusikiliza wanapojadili ombi la Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Palestina imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa lakini kwa ngazi ya muangalizi na sasa uongozi wa Palestina inataka hadhi hiyo kubadilishwa na kuwa mwanachama kama wanachama wengine 193 wa Umoja wa Mataifa.
Wajumbe katika baraza hilo la UN katika mazungumzo yao watazingatia ombi la Wapalestina la mwaka 2011 baada ya ombi lililowasilishwa kwa njia ya maandishi wiki iliyopita na Bwana Riyad Mansour, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Palestina ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa.
Wakati tukisubiri kusikia nini kitajadiliwa na Baraza hilo, huko Ukanda wa Gaza hali bado si hali kwani watoa misada ya kibinadamu wana wasiwasi mkubwa juu ya uvamizi unaopangwa kufanywa na Israel katika eneo la Rafah ambalo limefurika wapalestina waliokimbia kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo kusini, kati na kaskazini mwa Gaza kufuatia mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na wanajeshi wa Israel.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick, akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa hapo jana alisema kuwa “Mpango unaendelea wa uvamizi wa Rafah, ambao unaweza kusababisha hadi watu 800,000, kuyakimbia makazi yao…. Tulipata tabu sana kuleta mahitaji muhimu hapa kama vitu ambavyo si vyakula, malazi, nyenzo mbalimbali na maji…. Hatuna tena uwezo na rasilimali kwa sasa. Na tunatatizika sana kujiandaa.”
Ili kuongeza kiwango cha usaidizi wa kibinadamu kufika eneo hilo, Umoja wa Mataifa unaunga mkono wito wa bandari ya Ashdod ya Israel kufunguliwa tena hulo kaskazini mwa Gaza, ili misaada zaidi ipatikane kupitia nchi ya Jordan.
Mon, 08 Apr 2024 - 11593 - UNICEF na jitihada za kuimarisha huduma za Afya ya Akili kwa vijana nchini Rwanda
Makala hii inaeleza safari ya matumaini na uthabiti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNICEF Rwanda linaposhirikiana na Rwanda Biomedical Center (shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya) kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya akili kwa vijana. Katika mpango huu wa kutia moyo, UNICEF inavunja vizuizi na kukuza ujasiri kwa kutoa usaidizi muhimu kama vile nasaha shuleni
Fri, 05 Apr 2024 - 11592 - Mlo shuleni wawawezesha wasichana kuepuka ndoa za utotoni Sudan Kusini
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni.
Sudan Kusini ni moja kati ya mataifa yenye viwango vya chini vya watu wanaojua kusoma na kuandika hususani kwa wasichana. Jamii katika taifa hilo la afrika ya mashariki huwaoza mabinti ikiwa ni njia moja wapo ya familia kujipatia mali na hivyo mtoto wa kike hujikuta akikosa haki yake ya msingi ya kupata elimu.
Huko Kapoeta Mashariki katika jimbo la Equatoria mashariki, shule moja ya msingi ambayo hatutaitaja jina imekuwa kimbilio la wasichana walio katka hatari ya kuolewa katika umri mdogo, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo ni Grace mwenye umri wa miaka 16 anasema shule hiyo imekuwa nikama peponi.
“Nilipokuwa kijijini, wakati baba yangu alikuwa hai, maisha yalikuwa sawa na nilifurahia kila kitu maishani. Lakini mara baada ya baba yangu kufariki, hapo ndipo maisha yangu yakawa magumu, kaka yangu alitaka niolewe katika umri mdogo, na hapo ndipo maisha yakawa magumu”.
Grace anasema anachosikita ni kuwa watoto wa kike hawaheshimiki.
“Kwa sababu mimi ni mtoto wa kike maisha ya kijijini sio mazuri, tunatazamwa kama chanzo cha utajiri, na sisi ndio tunalazimika kufanya kazi za mashambani, kitu chochote kinachohusiana na shule hakithaminiwi, na hawataki hata kujua ni nini. Wao wanaona kama kitu kisicho na maana, hawajui chochote kuhusu elimu, na hawako tayari kwa hilo”.
Hellen Locham ni mwalimu wa shule anayosoma Grace na anasema wamekuwa wakihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa shule kwa wasichana.
“Hawa wasichana wanaitwa "washindi" kwa sababu wasichana hawa wanalazimishwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 9, na wengine huposwa wangali wadogo, na walifanikiwa kukimbia vijijini, wakiteseka njiani na wamefanikiwa kuja shuleni”. Tumekuwa tukiwaambia watu ikiwa unapata msichana ambaye anapitia changamoto, msichana ambaye amelazimishwa kuolewa, wanaweza kupata elimu wanayotaka".
Mwalimu Hellen Locham anasema mbali na shule kupokea wasichana lakini wanalishukuru zaidi shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani kwa kuwawezesha kupata chakula shuleni.
Chakula kuwa shuleni ni muhimu sana, ikiwa hakuna chakula na haujala kitu huwezi kuwa katika nafasi ya kuwa darasani, huwezi kufanya chochote, WFP imesaidia sana shule hii, wakati wa likizo hali inekuwa ngumu kwa wasichana hawa kuwa shuleni ikiwa hakuna chakula. Wengi wao wangaliweza kukimbia, wangaliweza kurudi makwao, wangesema bora niende kuteseka kuliko kufa hapa kwa njaa.
WFP inaendelea kusaidia wasichana walio hatarini zaidi kwa kuwaatia msaada wa chakula shuleni wakati wa likizo.
Fri, 05 Apr 2024 - 11591 - 05 APRILI 2024
- Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Rwanda kusikia programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Rwanda kudhibiti tatizo la changamoto ya afya ya akili kwa vijana balehe.Na katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani”.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Fri, 05 Apr 2024 - 11590 - Kuelekea miezi 6 ya mzozo wa Gaza, Guterres apinga matumizi ya akili mnemba kusaka wahalifu
Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.
Guterres akianza hotuba yake kwa kuelezea kuwa Jumapili hii inatimu miezi sita tangu mashambulizi hayo na kuelezea kuwa tarehe 7 Oktoba ni siku ya machungu kwa Israel na dunia, kwani Umoja wa Mataifa na yeye binafsi wanaomboleza vifo vya waisrael 1,200 waliouawa hadi sasa. Hakuna kinachohalalisha mashambulizi yale ya Hamas, amesema Guterres akisema pia katika kipindi cha miezi sita pia wapalestina zaidi ya 32,000 wameuawa na wengine zaid iya 75,000 wamejeruhiwa. Maisha ya watu yametwamishwa na heshima ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu imesambaratishwa.
Akarejelea ziara yake ya hivi karibuni kwenye kivuko cha Rafah ambako anasema nilikutana na wasaidizi wa kiutu wabobezi walionieleza wazi kuwa janga hili na machungu ya Gaza si ya kawaida na hawajawahi kushuhudia kokote.
Na zaidi ya yote anasema aliona misururu mirefu ya malori yenye shehena za misaada yakiwa yamezuiwa kuingia Gaza.
Anasema pindi milango ya misaada inapofungwa, milango ya njaa inafunguliwa. Zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na njaa. Watoto hivi sasa wanakuga kwa njaa na kukosa maji. Hakuna kinachohalalisha adhabu hii ya jumla kwa wananchi wa Palestina.
Ameelezea pia kuchukizwa na kitendo cha Israel kutumia Akili Mnemba kusaka wahalifu Gaza tena kwenye maeneo yenye watu wengi.
Akili Mnemba inapaswa kutumika kwa manufaa na sio kuchangia kwenye kusongesha vita.
Amekumbusha kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia na waandishi wa habari nao wameuawa kwenye mzozo huo. Na zaidi ya yote.
Vita dhidi ya habari imeongeza machungu.. kuficha ukweli na kurushiana lawama. Kuwanyima waandishi wa habari wa kimataifa kibali cha kuingia Gaza kunaruhusu kusambaa kwa habari potofu na za uongo.
Ametamatisha hotuba yake ya dakika 7 kwa kutaka pia uchunguzi huru wa kilichotokea Gaza, utekelezaji wa kikamilifu wa azimio la wiki iliyopita la Baraza la Usalama la kutaka sitisho la mapigano na misaada ifikie walengwa kwani baa la njaa linajongea Gaza.
Fri, 05 Apr 2024 - 11589 - Ujumuishwaji wa wanawake katika huduma za kifedha ni muhimu - Nangi Massawe, Benki Kuu Tanzania
Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo.
Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha.
Thu, 04 Apr 2024 - 11588 - Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri.”Thu, 04 Apr 2024
- 11587 - 04 APRILI 2024
- Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na msaada wa kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mabomu, vilipuzi na vifaa vingine vya mlipuko vinaendelea kuua na kujeruhi watu katika maeneo mengi yenye changamoto kubwa za migogoro duniani na matokeo yake vifaa hivyo vya mlipuko, kwa wastani hukatili maisha ya mtu mmoja kila saa, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick anaelekea Gaza leo. Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza. Mfumo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) wa Ufuatiliaji kuhusu Mashambulizi dhidi ya Huduma za Afya (SSA) wameeleza kuwa inatia wasiwasi kwamba nchini Ukraine wahudumu wa afya katika gari za wagonjwa na wafanyakazi wengine wanaotoa huduma za usafiri wa afya wanakabiliwa na hatari ya kujeruhiwa na kifo mara 3 zaidi ya ile ya wafanyakazi wengine wa huduma za afya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 04 Apr 2024 - 11586 - UNCTAD, UNECA, Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.
Kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi ya Afrika UNECA, Kenya inaunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara. Evarist Mapesa amefuatilia taarifa hiyo kwa kina na kutuandalia makala hii.
Wed, 03 Apr 2024 - 11585 - Mbinu za medani tulizopatiwa ni za kimataifa- Afisa FARDC
Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Je, FARDC linajengewa uwezo gani? Assumpta Massoi anafafanua zaidi.
Hapa si uwanja wa vita bali ni uwanja wa mazoezi! Wanajeshi 30 wa FARDC au jeshi la serikali nchini DRC wakiwa kwenye mafunzo ya kulenga shabaha. Mbele kuna karatasi lililochorwa binadamu na sasa wanatakiwa kulenga maeneo mbali mbali ya mwili yaliyowekwa alama.
Ni mbinu wanazopatiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Brazil, hapa Beni jimboni Kivu Kaskazini ili waweze kukabiliana na waasi kwenye maeneo misituni. Kapteni Rombaut Mukoka ni Afisa wa jeshi la FARDC na anasema, “Mafunzo haya ni muhimu sana. Yanapaswa kuendelea ili hatimaye wanajeshi wetu waweze kunufaika. Hizi mbinu walizojifunza ni mpya sana kwetu na zinatambulika katika medani za kimataifa.”
Mafunzo ya kulenga shabaha yanaendelea na kisha mkufunzi kutoka Brazil anajongea kwenye picha ile akiwa na mmoja wa wanafunzi ili kuonesha ni wapi haswa wanapaswa kulenga.
Jenerali Luciano Alfred Matamba ni Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha MONUSCO mjini Beni na anafafanua lengo la mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwapatia mbinu na ufundi za kuendesha operesheni msituni. Kama unavyofahamu hapa Kivu Kaskazini tuko kwenye eneo la operesheni ambalo kwa kiasi kikubwa ni pori na mashambulizi yanayofanywa na waasi wa ADF yanahitaji mbinu mtu kuwa na hizo mbinu za kupigana msituni. FARDC [EF EI AR DE SE] ni wadau wetu ambao tunapaswa kushirikiana nao kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa namba 2717 [Mbili Saba Moja Saba]. Ni pale tu ambapo tutajifunza pamoja na kuwa na mbinu sawa ndio tutaweza kutatua matatizo yaliyoko hapa.”
Wed, 03 Apr 2024 - 11584 - 03 APRILI 2024
- Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Makala inatupeleka nchini kenya ambako serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaunda viashiria vipya ya kupima usawa wa kijinsia katika biashara.Na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo miradi ya maji mkoani Kigoma inavyowasaidia wanfunzi.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wed, 03 Apr 2024 - 11583 - UN - Bila usitishaji mapigano hali ya kibinadamu inaendelea kuwa tete Gaza
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.
Asante Anold kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA usiku wa kuamkia leo makombora ya Israel yameendelea kuvurumishwa kuelekea Gaza Kaskazini, Khan Younis na Rafah ambako takriban Wapalestina milioni 1.2 sasa wanaishi katika makazi rasmi na yasiyo rasmi na hivyo kuwaongezea hofu ya mustakbali wa maisha yao.
Pia shirika hilo linasema fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji mkubwa bado ni mtihani hasa kutokana na mamlaka ya Israel kuendelea kulinyima vibali shirika la UNRWA kufikisha msaada muhimu wa chakula na mahitaji mengine hasa Gaza Kaskazini.
Hatua hiyo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA imezidisha njaa kwa watu ambao tayari wako taaban na mapigano yanayoendelea.
Tangu Machi mosi OCHA inasema Israel imekataa kuruhusu asilimia 30 ya operesheni za kibinadamu Gaza Kaskazini na kuathiri kwa kiasi kikubwa operesheni za UNRWA.
Watoto 27 wameripotiwa kufa njaa kutokana na utapiamlo hadi sasa huku shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF likionya kwamba Maisha ya maelfu wengine yako hatarini ukizingatia ukweli kwamba tangu Oktoba 7 mwaka jana watoto zaidi ya 13,000 wameuawa kutokana na vita inayoendelea lakini njaa nayo ni tishio kubwa.
Kuhusu uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita inayoendelea ripoti ya pamoja ya tathimini ya Umoja wa Mataifa na Benk ya Dunia iliyotolewa leo inasema uharibifu huo unakadiriwa kuwa takriban dola bilioni 18.5 ambao ni sawa na asilimia 97 ya pato la taifa la Ukingo wa Magharibi na Gaza kwa mwaka 2022.
Na hapa Makao Makuu leo Umoja wa mataifa umepokea barua rasmi kutoka kwa mamlaka ya Palestina ikiomba kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa badala ya nafasi ya uangalizi iliyonayo sasa.
Wed, 03 Apr 2024 - 11582 - Bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kote duniani - Paulina Ngurumwa
Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme.
KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Tue, 02 Apr 2024 - 11581 - 02 APRILI 2024
- Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika lisilo la kiselikali au NGO la World Central Kitchen yaliyofanywa na jeshi la Israel, maafisa hao wakirejea kueleza hofu yao kwamba hakuna mahali palipo salia kuwa salama Gaza.Tume ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya UNJHRO imesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC. Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimishana kuhusu usonji maudhui yakiwa kutoka kuishi kuelekea kwenye ustawi, kwa watu wenye usonji au kwa kiingereza Autism, ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, usonji hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani.Na mashinani tunaelekea Gaza kuona ni kwa jinsi gani mashambulizi ya Israel ya hivi majuzi yameathiri huduma za afya katika hospitali ya Al-Shifa.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 02 Apr 2024 - 11580 - Mradi wa maji warejesha matumaini kwa familia Wajir
Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka. Lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na serikali ya Kaunti walianzisha mradi wa ujenzi wa kuchimba visima wa Giriftu kwa ili jamii iwe na uhakika wa kupata maji wakati wowote. Mradi umezaa matunda na ndio msingi wa makala yetu ya leo inayoletwa na Assumpta Massoi.
Mon, 01 Apr 2024 - 11579 - Griffiths: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome
Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.
Bwana Griffiths ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter akisistiza kuwa juhudi zozote za kusambaza misaada ya kibindamu kwenye Ukanda wa Gaza bila kupitia shirika la UNRWA haziwezi kufanikiwa na watu zaidi ya milioni 2 wanaitegemea UNRWA ili kuendelea kuishi.
Ameendelea kusema kwamba hadi sasa hakuna shirika lingine lolote lenye uwezo wa kufika kila kona ya Gaza, uzowefu na imani ya jamii ya kutekeleza majukumu yake kama lilivyo shirika la UNRWA.
Wakati huohuo shirika la UNRWA limeonya kwamba mashambulizi ya Israel yameendelea tena usiku wa kuamkia leo huko Gaza Kaskazini Khan Younis na Rafah ambako watu milioni 1.2 wanapata hifadhi na kusababisha vifo zaidi.
Huku lile la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema wakati timu yake ikiwa katika operesheni ya kibinadamu katika hospital ya Al-Aqsa jana Jumapili maeneo ya hospital yalipigwa na shambulio la anga lililokatili maiasha ya watu 4 na kujeruhi wengine 17.
Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linajitahidi kwa kila hali kutoa msaada wa chakula unaohitajika sana kwa watu milioni 1.45 Gaza lakini msaada huo hautoshi na bila usitishaji vita hawawezi kumfikia kila mtu na hivyo kufanya Maisha ya watu wengi kusalia hatarini.
Mon, 01 Apr 2024 - 11578 - 01 APRILI 2024
- Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya, anakupeleka kaunti ya Wajir kuona jinsi mradi wa maji ulivyoleta matumaini kwa familia na jamii.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu afya kwa watoto.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Mon, 01 Apr 2024 - 11577 - Kituo cha amani DR Congo chakabili habari potofu na za uongo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika.
Jean Claude Batumike, ambaye ni Mkuu wa kituo cha vijana cha Amani, kilichoko eneo la Kamanyola huko jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza kupitia video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagramanasema kituo hicho kilipojengwa watu walijihisi wako na amani zaidi.
Anasema kituo cha amani kilijengwa kwa ajili ya amani ili kuondoa migogoro kwa vijana na jamii kwa ujumla. Kituo kina kompyuta, mtandao wa intaneti wakati wote na skrini kubwa ambapo katika video hiyo wanaonekana vijana wakipita hapa na pale huku wakipatiwa maelezo na Bwana Batumike.
Akilinganisha hali kabla na baada ya kujengwa kwa kituo hicho, Bwana Batumike anasema, “mara nyingi wakati tulikuwa na mizozo hapa kwenye eneo letu, hakukuweko na mahali ambapo watu wanaweza kwenda na kutatua mizozo, lakini tangu wamejenga hiki kituo cha Amani, kushikakuweko na mzozo wa vijana au jamii, wanakimbilia kituo cha Amani, wanakaa pamoja na kutatua mizozo na hatimaye mambo yanakuwa mazuri zaidi.”
Bwana Batumike akaelezea kuwa kituo cha Amani kinasaidia kukabili habari za uongo na potofu kwa kuwa kituo kina mtandao wa uhakika wa intaneti, kompyuta na skrini na wanaweza kupata habar iza ukweli.
“Mara nyingi vijana wanapokuwa na habari za wasiwasi ambazo hawana uhakika nazo ni rahisi kufika kituo cha Amani, wanajiunganisha kwenye intaneti, wanarambaza na kusogoa na wengine kwa mtandao na kupata habari za ukweli. Na katika sehemu yenye mzozo, unahitaji kupata habari za uhakika,” anasema Bwana Batumike.
Mon, 01 Apr 2024 - 11576 - Kituo cha malezi ya watoto nchini Kenya chatekeleza azma ya Umoja wa Mataifa
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira.
Umoja wa Mataifa unasema kila mtu ana haki ya elimu hata kama amepata changamoto gani maishani. Na ndipo ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia lile la “Work for life”, pamoja na lile la “A Pack a Month”, linalohusika na utoaji wa misaada mbali mbali ikiwemo taulo za kike kwa wazazi wenye mahitaji na wasichana wanaokwenda shule walizindua kituo cha malezi ya watoto wachanga nyakati za mchana katika eneo la Ngong nchini Kenya. Mradi unaungwa mkono na wadau kadhaa ikiwemo serikali ya Kenya. Selina Jerobon ni msimulizi wetu kupitia mada hii iliyofanikishwa na Redio washirika DOMUS ya huko Kenya.
Thu, 28 Mar 2024 - 11575 - Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “UDENDA”Thu, 28 Mar 2024
- 11574 - 28 MACHI 2024
- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) leo Machi 28 limetahadharisha kuhusu ujio wa baa la njaa katika Ukanda wa Gaza. UNRWA imesema yenyewe ni uti wa mgongo wa misaada ya kibinadamu Gaza lakini bado misafara yao ya chakula imezuiwa kufika kaskazini, ambako baa la njaa linajongea. Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limesema kati ya hospitali 36 katika Ukanda wa Gaza, ni 10 tu ambazo zimesalia zikifanya kazi japo nazo kwa kiasi kidogo.Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inataka hatua za haraka na za ujasiri ili kukabiliana na hali ya "janga" nchini Haiti. Ripoti imeeleza kuwa magenge yanaendelea kutumia unyanyasaji wa kingono kuwatendea unyama, kuwaadhibu na kuwadhibiti watu. Wanawake wamebakwa hata baada ya kushuhudia waume zao wakiuawa mbele yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), pamoja na wadau wake 123, Alhamis ya leo limetangaza kuwa linatafuta dola bilioni 1.4 mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini wanaoishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda. Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini linasalia kuwa ndilo kubwa zaidi barani Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 28 Mar 2024 - 11573 - Simulizi za raia wanaokimbia mashambulizi kaskazini mwa MsumbijiWed, 27 Mar 2024
- 11572 - Innoss B kushirikiana na WFP kusongesha lishe na elimu DRC
Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Nimeshuhudia njaa mara nyingi sana wakati wa utoto wangu, kabla ya kwenda shule tulikuwa na njaa na kabla ya kulala tulikuwa na njaa, ndivyo asemavyo mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ambaye ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Taarifa ya WFP iliyotolewa Kinshasa, mji mkuu wa DRC imemnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain akisema “ninafurahia sana kumkaribisha kwenye timu yetu ya WFP, tukiwa na Innos tutaweza kuwa na athari chanya kwenye vita dhidi ya njaa na utapiamlo DRC.”
Innos amenukuliwa akisema njaa ilikuwa sehemu ya maisha yake wakati akiwa mtoto na kwamba “kila siku unalazimika kufirikia leo nitakula vipi? Nitapataje chakula hii leo? Hakukuwa na matumaini.”
Sasa mwanamuziki huyu aliyejipatia umaarufu sio tu nchini mwake bali pia Afrika na dunia nzima kutokana na mitindo yake ya AfroBeat na Rumba amepatiwa jukumu na WFP kutumia muziki wake kuelimisha jamii umuhimu wa lishe bora na elimu nchini mwake DRC.
Innos ambaye ni mzaliwa wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, anasema njaa ilikuwa kichocheo cha muziki na hivyo aliona ana deni kwa jamii yake ya kusaidia kuongeza uelewa na hamasa kuhusu tatizo hilo.
Kupitia video ya WFP Innoss’B akiwa kwenye moja ya mashamba ya mboga za majani nchini DRC, akiambatana na wanawake na kwingine akiwa na wanafunzi anasema, “leo nina furaha kwa sababu kwa mara moja nina fursa ya kuwa karibu na jambo ambalo linanigusa mno. Kuhakikisha kila mtu ana afya njema . Kuhakikisha kila mtu ana nguvu, kuhakikisha kila mtu anaweza kupata chakula. Ujumbe huo utasikika . Hivyo niña furaha sana, hii itakuwa ni safari nzuri. Nina furaha.”
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, ambaye kwa mara ya kwanza alikutana na Innoss’B mjini Goma, miaka 14 iliyopita, wakati huo Innoss akiwa na umri wa miaka 13, amesema amekuwa anajivunia sana kuona kila kitu alichofanikiwa kama msanii na msongeshaji wa utu wa kibinadamu.
Amesema kujituma kwake katika kujenga mustakabali bora kwa wananchi wa DRC ni hamasa ya dhati.
Innos anasema anaamini kwenye nguvu ya muziki na utamaduni katika kuleta mabadiliko chanya. Kushirikiana na WFP kunaniruhusu kuchangia katika kutatua masuala nyeti ya lishe na elimu nchini mwangu. Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko yenye maana kwa maisha ya vijana.”
Peter Musoko ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini DRC anasema wanafuraha kubwa kushirikiana na Innos’B na kutumia nguvu ya muziki kusongesha ustawi wa DRC na wananchi wake. “Kwa kuunganisha nguvu, tunaweza kuchochea hatua chanya na kutatua changamoto kubwa ya utapiamlo na ukosefu wa uhakika wa chakula.”
Wakati huu ambapo WFP inaendelea na jitihada za kuimarisha uhakika wa kupata chakula DRC, ushirikiano na Innoss’B unaongeza sauti muhimu katika kampeni hiyo.
Hata hivyo WFP inasema ukata ni tatizo kwa sasa kwani bajeti yake kwa DRC ina pengo la dola milioni 548.5, fedha ambazo zinahitajika kwa kipindi cha miezi sita ijayo kuweza kukidhi mahitaji ya kiutu yanayoongezeka kila uchao.
Wed, 27 Mar 2024 - 11571 - 27 MACHI 2024
- Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunaangazia mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mlinda amani wa kuhusu elimu kwa wasichana.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Wed, 27 Mar 2024 - 11570 - WHO Zambia yashirikiana na Serikali kutokomeza Kipindupindu
Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.
Jioni moja Philta Samazimva alilalamika ghafla tumbo kuuma, baada ya kuharisha sana, mama yake mzazi Hildar Samazimba alimpeleka kliniki.
Baadhi ya watu hapa walisema usiende hospitali mtoto atapona, hakuna kitu watakachompatia mtoto na atakufa. Lakini nilipoona jinsi mtoto wangu alivyokuwa anaonekana, nilisema wacha niwahi kliniki.
Philta alipelekwa kwenye kituo cha matibabu cha Heroes Cholera, ambapo alipata ahueni baada ya matibabu. Dr Mavis Chisala, Ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika kituo cha kutibu kipindupindu cha Mashujaa.
"Tumekuwa tukihakikisha tunamfuatilia mgonjwa wetu, kwa sababu kwa watoto wanaimarika haraka sana unapochukua hatua sahihi kwa wakati muafaka.
Kiwango cha vifo vya wagonjwa wa kipindupindu katika vituo vya afya ni asilimia 1.3, ikilinganishwa na asilimia 3.3 kwa ujumla, kutokana na kazi inayofanywa na matabibu hao kwa ushirikiano na WHO ambao umerejesha matumaini kwa Samazimba
“ kikubwa tulifanya kazi kwa ushirikiano, ninawashukuru Wauguzi, matabibu kwa kazi waliyoifanya, kwasababu sikujua kama mtoto wangu atapona
WHO imeisaidia wizara ya afya nchini Zambia kurekebisha miongozo ya huduma za kliniki na kununua vifaa tiba na vifaa vingine kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu. Dkt. Kalima Nawa, kiongozi mkuu wa kituo cha matibabu cha mashujaa wa kipindupindu anasema Hold under……03 sec “tunatarajia kuendelea kufanya kazi na WHO katika mlipuko huu, na pia kupanga kwa ajili ya milipuko ya baadaye na kutusaidia kujiandaa kwa hayo”.
Kipindupindu kinatibika kwa urahisi iwapo kitagunduliwa kwa wakati.
Wed, 27 Mar 2024 - 11569 - 26 MACHI 2024
- Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kutokana na ongezeko la hatari kwa watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Na wakati mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) unaohusu Wahamiaji Wasiofahamika waliko ukitimiza miaka kumi, ripoti mpya ya shirika hilo iliyopewa jina ‘Muongo mmoja wa kukusanya taarifa za vifo vya wahamiaji’ inaonesha mienendo ya kutisha ya vifo na kupotea kwa wahamiaji katika muongo mmoja uliopita na kwamba mtu mmoja kati ya watatu hufariki duniani katika harakati za kukimbia migogoro katika nchi yake.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Mhandisi Denis Arbogast, Msimamizi wa mradi wa maji Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania, mradi inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Tue, 26 Mar 2024 - 11568 - Nyumba salama kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono Sudan Kusini
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Leah Mushi na maelezo zaidi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa zamani wa UNMISS ofisi ya Yambio, Christopher Muchiri Murenga, mradi huu ulioanzishwa na kitengo cha ushauri cha ulinzi wa wanawake cha UNMISS na umefadhiliwa na Muungano wa Ulaya pamoja na Shirika la Rural Action Aid lengo likiwa ni kuwasaidia waathirika wa unyanyasji wa kijinsia unaohusiana na migogoro.
Bwana Murenga anasema,“kama sehemu ya kutafuta amani ya kudumu na jumuishi nchini Sudan Kusini, imebidi tuwalete manusura pamoja ili waweze kuponya majeraha yao. Kisha watakuwa wanajamii wenye tija, wakichangia ustawi wa kijamii na kiuchumi wa serikali.”
Kituo hiki kinatoa ushauri nasaha, kuponya watu wenye kiwewe pamoja na mafunzo ya stadi za maisha na kinalenga kusaidia manusura 195. Mmoja wa wanufaika ni Azande ambaye katika video ya UNMISS amefichwa sura yake wakati akieleza masahibu aliyopitia akisema, “tulipotoka porini nilikuwa na kiwewe, walitupa ushauri nasaha na mawazo yote mabaya yaliyokuwa akilini mwangu yaliondoka na sasa niko thabiti zaidi. Mimi ni miongoni mwa wale ambao sasa wanajifunza ushonaji. Wakati nipo msituni nilijifungua mtoto wa kike sasa ana umri wa miaka 6. Ana matatizo ya tumbo kwa sababu wakati mjamzito nilikuwa nakula vitu vya hatari ndio maana sasa naomba msaada wa dawa kwa ajili yake.”
Kiongozi wa kikundi cha wanawake katika eneo la Ezo Henrica Elias anasema nyumba hii itasaidia wasichana na wanawake wengi sana kwa kuwa, “kituo hiki ni kama ndoto inayotimia, imetuletea furaha ambayo hatuwezi kuieleza. Yaliyotusibu sisi wanawake na wasichana wakati wa mzozo ni yakutisha. Mambo mengi mabaya yalitendeka katika vijiji vyetu, ambapo wasichana wadogo na wavulana pia walitekwa nyara.”
Migogoro nchini Sudan Kusini imesababisha tajriba ya kuhuzunisha kwa vijana wengi wa kike na wa kiume, hasa wale ambao walilazimika kujiunga na makundi yenye silaha nchini humo.
Mon, 25 Mar 2024 - 11567 - Guterres: Tekelezeni kikamilifu mkataba wa mwaka 1994 wa kuwalinda wafanyakazi wa UN
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu kuenzi ujasiri na kujitolea kwa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kila mahali kokote waliko kwa kuahidi kuwalinda na kuwaunga mkono wanaposaidia kujenga dunia yenye amani zaidi na ya utu kwa ajili ya watu wote. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Siku hii ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko huadhimishwa kila mwaka Machi 25 katika kumbukumbu ya kutekwa nyara kwa Alec Collett, mwandishi wa habari wa zamani ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wakati alipotekwa nyara na mtu aliyekuwa na silaha mwaka wa 1985 na baadaye mwili wake kupatikana katika Bonde la Bekaa nchini Lebanon mwaka wa 2009 yaani miaka 24 baadaye.
Maadhimisho ya siku hii, katika miaka ya hivi karibuni yamekuwa hata ana umuhimu mkubwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu Guterres kupitia ujumbe wake kwa maadhimisho ya mwaka huu anatoa takwimu za hivi karibuni akieleza kwamba tangu mwaka juzi 2022, wafanyakazi 381 wa Umoja wa Mataifa wamewekwa kizuizini ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 7 mnamo mwezi Januari na Februari mwaka huu 2024. Kwa jumla, wafanyakazi 27 wa Umoja wa Mataifa bado wako kizuizini.
Bwana Guterres anasema leo ni ukumbusho mzito wa hatari kubwa zinazowakabili wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanapofanya kazi yao muhimu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwamba, "Mioyo yetu iko pamoja na familia zao na wafanyakazi wenzao”, na kwamba hatakataa tamaa kutaka waachiliwe na kurudi salama."
Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anazisihi nchi zote kutekeleza kikamilifu Mkataba wa mwaka 1994 wa Usalama wa Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Washirika wao, na pia Itifaki ya Hiari ya mwaka 2005 ya Mkataba huo.
Mon, 25 Mar 2024 - 11566 - 25 MACHI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akianzia na siku ya kimataifa ya kukumbuka watumishi wa UN wanaoshikiliwa vizuizini na wasiofahamika waliko, kisha anakwenda Sudan Kusini na harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono. Makala ni harakati za kumkomboa mwanamke na mashinani arejea Sudan Kusini.
- Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu kuenzi ujasiri na kujitolea kwa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kila mahali kokote waliko kwa kuahidi kuwalinda na kuwaunga mkono wanaposaidia kujenga dunia yenye amani zaidi na ya utu kwa ajili ya watu wote. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya ambako mkutano wa maandalizi wa asasi za kiraia umekunja jamvi hivi karibuni na Stella Vuzo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi alizungumza na Carole Osero-Ageng'o Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo. Anazungumzia harakati za kumkomboa mwanamke.Mashinani ni mlinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kutoka taifa la Bhutan.
Mon, 25 Mar 2024 - 11565 - Maji yanaweza kuleta amani au kuchochea migogoro
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Maji, Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM ya nchini Kenya amezungumza na baadhi ya wakazi wa Kaunti ya Kajiado nchini humo kuhusu umuhimu wa uwepo wa maeneo mengi ya kupata maji katika jamii. Dhima ya Siku ya Kimataifa ya Maji ya mwaka huu wa 2024 ni "Maji kwa ajili ya amani" ikieleza kuwa kunapokuwa na ushirikiano katika suala la maji inaleta athari chanya kukuza maelewano, kuhamasisha ustawi na kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto za pamoja.
Fri, 22 Mar 2024 - 11564 - 22 MACHI 2024
Hii leo jaridani ikiwa ni Siku ya maji duniani, tunaangazia utunzaji wa vyanzo vya maji. Pia tunamulika mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 ambao umekunja jamvi hii leo. Makala tuankupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania kufuatilia jinsi ambayo miradi ya maji inavyoleta manufaa kwa jamii.
- Leo ni siku ya maji duniani chini ya kauli mbiu Maji kwa amani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza nchi kuhakikisha zinashirikiana na kuwa na makubaliano ya kutumia vyanzo vya maji.Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 umekunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataia jijini New York, Marekani na miongoni mwa washiriki ni Matika Maiseli, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Afya na Mimea na Viuatilifu, TPHPA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo nchini Tanzania. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ubaguzi wa rangi ni jinamizi linaloathiri nchi na jamii kote duniani chimbuko lake likitokana na sera za ukoloni na utumwa. Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi hii leo inayojikita na mada ya watu wenye asili ya Afrika katika kutambuliwa kwao, kupewa haki na maendeleo, ametaka kutokomezwa kwa jinamizi hilo kwani linapokonya fursa, kunyima utu, kukiuka haki, kupora maisha na pia kuyaharibu.Katika mashinani tutakupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo miradi ya maji imeleta nafuu kwa jamii.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Fri, 22 Mar 2024 - 11563 - Tunawezesha wakulima wanawake Tanzania ili wapate masoko ndani na nje ya nchi - Matika Maiseli, TPHPA
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 umekunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataia jijini New York, Marekani na miongoni mwa washiriki ni Matika Maiseli, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Afya na Mimea na Viuatilifu, TPHPA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo nchini Tanzania.
Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye kufahamu ni nini anaondoka nacho kutoka mkutano huu uliolenga kusongesha usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na kutokomeza umaskini.
Fri, 22 Mar 2024 - 11562 - Umoja wa Mataifa yataka nchi kuwa na makubaliano ya ushirikiano wa matumizi ya vyanzo vya maji
Leo ni siku ya maji duniani chini ya kauli mbiu Maji kwa amani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza nchi kuhakikisha zinashirikiana na kuwa na makubaliano ya kutumia vyanzo vya maji.
Katika ujumbe wake huo Guterres ameeleza kuwa mpaka sasa ulimwenguni “Nchi 153 zinashirikiana vyanzo vya maji lakini ni nchi 24 pekee zenye makubaliano kwa vyanzo vyao vyote vya maji wanavyoshirikiana.”
Amesema hali haipaswi kuwa hivyo na nchi zinatakiwa “kutekeleza Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa ambao lengo lake ni kuhamasisha usimamizi wa rasilimali za maji za pamoja kwa njia endelevu.”
Hii leo kukiwa na mikutano mbalimbali pamoja na ripoti za mashirika ya Umoja wa Mataifa, kimataifa, kitaifa na asasi za kiraia zinazoelezea matumizi ya maji pamoja na changamoto zake ulimwenguni, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametaka watu wote kutambua kwamba kushirikiana katika kulinda vyanzo vya maji kunaweza kuimarisha na kudumisha amani.
Kama Kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema “Maji kwa amani” Guterres amesema “Hatua zinachokuliwa kwa ajili ya maji ni hatua kwa ajili ya amani na hii inahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Usimamizi wa maji unaweza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na uhusiano kati ya jamii, na kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga yaletwayo na mabadiliko ya tabianchi. Unaweza pia kuendeleza maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs ambayo ni msingi wa jamii zenye amani, ikiwa ni pamoja na kuboresha afya, kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa, na kuimarisha usalama wa chakula na maji.
Amehitimisha kwa kutoa wito kwa jamii yote kujitolea kufanya kazi pamoja, kufanya maji kuwa nguvu ya ushirikiano, maelewano na utulivu, na hivyo kusaidia kuunda ulimwengu wa amani na ustawi kwa wote.
Fri, 22 Mar 2024 - 11561 - Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Panda"Thu, 21 Mar 2024
- 11560 - 21 MACHI 2024
- Wakati hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbayá Gaza mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la afya duniani WHO yamerejea wito wa kutaka kusitishwa mapigano mara moja na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaingia Gaza ambako maisha ya zaidi ya watu milioni 1 yako hatarini kwa njaa..Leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa unaoathiri uwezo wa mtu kujifunza au downsyndrome mwaka huu ikibeba maudhui ya kutokomeza unyanyapaa yakimchagiza kila mtukuwajumuisha watu wenye downsyndrome kwenye nyanja zote za maisha na kutowabagua. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ubaguzi wa rangi ni jinamizi linaloathiri nchi na jamii kote duniani chimbuko lake likitokana na sera za ukoloni na utumwa. Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi hii leo inayojikita na mada ya watu wenye asili ya Afrika katika kutambuliwa kwao, kupewa haki na maendeleo, ametaka kutokomezwa kwa jinamizi hilo kwani linapokonya fursa, kunyima utu, kukiuka haki, kupora maisha na pia kuyaharibu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya neno “PANDA”
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Thu, 21 Mar 2024 - 11559 - Watoto Gaza waamua vita isiwe sababu ya kunyong’onyea wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
Huko Ukanda wa Gaza, vita inayoendelea tangu Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya Hamas kurusha makombora Israel na kisha Israel kuamua kujibu mashambulizi licha ya kusababisha vifo vya watu 31,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, watoto waliosalia wameona mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani usipite hivi hivi. Wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Deir El Balah katikati mwa Gaza, watoto hao wameona furaha ni bora kuliko machungu ya njaa, ukimbizi, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii unaowakabili. Mwandishi wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza, Ziad Talib amefika hapo ili kufahamu hasa msingi wa hatua ya watoto hao na ndio makala ya leo inayosimuliwa na Assumpta Massoi.
Wed, 20 Mar 2024 - 11558 - WHO: Madaktari Gaza wanafanyakazi kutwa kucha kuokoa maisha bila kutia chochote tumboni
Wahudumu wa afya Gaza wanafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha wakihaha kuokoa Maisha ya wagonjwa na majeruhi katika hospitali chache zilizosalia zikifanyakazi bila kutia chochote tumboni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.
WHO inasema wafanyakazi hao wanaolazimika kufanyakazi saa 24 kuokoa maisha ya watu kama ambavyo wanakosa vifaa muhimu na vitendeakazi vingine vivyo hivyo wanakosa chakula cha kutosha kama ilivyo kwa maelfu mengine ya raia wa Gaza.
Timu ya WHO iliyozuru Hospitali ya Al-Aqsa katikati mwa Ukanda wa Gaza ili kupeleka vifaa muhimu imezungumza na wafanyakazi kuhusu hali zao, ikiwa ni pamoja na hali yao ya lishe.
Bashar Abdelkader, ambaye ni daktari wa kujitolea katika hospitali hiyo, amesema madaktari wanapewa chakula lakini wanakosa viambato muhimu vya lishe, hasa mchele na mboga nichache.
Ameongeza kuwa mlo mmoja unaweza kugawiwa kwa watu wawili na zaidi ya yote,chakula haitoshi kwa daktari wa zamu wanofanyakazi kwa saa 24 hospitalini hapo.
Tahani al-Samra, ambaye pia ni daktari wa kujitolea katika hospitali ya al-Aqsa amesema "Tunakabiliwa na utapiamlo na ukosefu wa nyenzo tunazohitaji. Kwa sasa hakuna mboga za asili za majani, matunda au virutubisho vingine muhimu. Tunategemea vyakula vya makopo, ambavo bei yake inapanda kwa kasi."
WHO na washirika wake wanafanya operesheni ya hatari kubwa wakihaha kupeleka dawa, mafuta na chakula kwa wahudumu wa afya na wagonjwa.
Lakini maombi ya ufikishaji wa bidhaa mara nyingi hukataliwa au kutatizwa. Uharibifu wa barabara na mapigano yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na ndani na karibu na hospitali, pia yanatatiza utoaji wa misaada.
WHO imeonya kwamba bila kuwepo hatua kubwa na za haraka za utoaji wa chakula, maji na vifaa vya msingi, hali ya Gaza, ambako njaa inaathiri karibu watu wote, karibu familia zote zinalazimika kuruka mlo kila siku na watu wazima wanapunguza kiwango cha ulaji wao wa kula.
Nusu ya watu wote ambao ni watu milioni 1.1 huko Gaza, wamechoka kabisa na hakuna usambazaji wa chakula na uwezo wao wa kukabiliana na njaa mbaya ni mdogo.
Umoja wa Mataifa unasema “Hii ndiyo idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika orodha ya watu wanaokabiliwa na njaa kali Gaza.”
Wed, 20 Mar 2024 - 11557 - 20 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya huduma za afya katika ukanda wa Gaza, na harakati za chanjo kwa watoto nchini Yemen. Makala tunasalia huko huko Gaza na mashinani inatupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu siku ya furaha duniani.
- Wahudumu wa afya Gaza wanafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha wakihaha kuokoa Maisha ya wagonjwa na majeruhi katika hospitali chache zilizosalia zikifanyakazi bila kutia chochote tumboni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.Katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen limekuja na mbinu ya kutumia watoto kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo. Makala inatupeleka Gaza huko Mashariki ya Kati kupata taswira tofauti na ile ambayo imezoeleka kwa takribani miezi sita sasa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na Ziad Talib, mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza.Katika mashinani ikiwa leo ni siku ya furaha duniani Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ameuliza wananchi furaha ina maana gani kwao.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Wed, 20 Mar 2024 - 11556 - UNICEF yatumia watoto kuhamasisha jamii kupata chanjo nchini Yemen
Katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen limekuja na mbinu ya kutumia watoto kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo.
Mtoto Leen mwenye umri wa miaka 10 kutoka nchini Yemen, anasema kupitia mpango wa ufadhili wa mtoto, programu inayotumia watoto kwenda kuhamasisha jamii kupata chanjo ili wawe na afya bora amefanikisha watoto 150 kupata chanjo katika jamii yake.
Akieleza hasa jumuku lake Leen anasema ‘Nawasisitiza walezi, umuhimu wa kupata chanjo na pia nacheza na watoto pale wanapokuwa wanachomwa sindano za chanjo ili kuwafanya wajisikie vizuri”
Katika kipindi cha miaka mwili UNICEF imefanikiwa kuwapatia mafunzo watoto 1000 ambao kwa pamoja wamefanikiwa kushawishi watoto 33,000 kupatiwa chanjo.
Watoto hao kama Leen huambatana na mtu mzima ambaye ni muhamasishaji wa jamii kwenda kuhamasisha familia kuhusu chanjo za kawaida ambazo watoto wanapaswa kupata.
Mmoja wa waliohamasishwa na mtoto Leen ni Somaia Mohammed, mama wa watoto watatu.
“Nilikuwa najizuia kwenda kuwapatia chanjo watoto wangu, hata hivyo baada ya Leen kunitembelea nyumbani kwangu baada ya mtoto wangu kuugua surau na kunielezea kama ningekuwa nimewapatia chanjo watoto wangu wasingeugua kiasi hicho nilihamasika na ushauri wao na kutembelea kituo cha afya kuwapatia chanjo watoto wangu.”
Na mtoto Leen anafurahi kuona jirani yake Somaia na watoto wake watatu wamepata chanjo baada ya kumtembelea mara kadhaa.
Anasema kati ya mambo aliyokuwa akimwambie wakati akienda kumhamasisha alikuwa akisema “Angalia nilivyo na afya bora na nilivyo na nguvu naweza kwenda shuleni sababu nimepata chanjo zote zinazohitajika”
Wed, 20 Mar 2024 - 11555 - 19 MACHI 2024
- Mashirika Umoja wa Mataifa yanayotoa msaada wa kibinadamu huko Gaza hii leo yamesisitiza azma yao ya kusaidia wakazi wa eneo hilo ambako watoto walio hatarini kufa kutokana na njaa kali iliyosababishwa na miezi mitano ya mashambulizi ya Israel na kushindwa kufikishiwa misaada inazidi kuongezeka.Mwaka 2023 ulikuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika rekodi zote zilizowahi kunukuliwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO katika ripoti yake iliyotolewa hii leo huko Geneva, Uswisi, rekodi za viwango vya joto ardhini, baharini zikivunjwa, barafu na theluji ncha ya kusini zaidi mwa dunia navyo vikiyeyuka. Na ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaonesha kitendo cha sekta binafsi kutumikisha watu huzalishafaida isiyo halali yad ola bilioni 236 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la asilimia 37 tangu mwaka 2014.Katika mashinani tutaelekea katika ukanda wa Gaza ambapo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, katika mwezi mmoja utapiamlo uliokithiri umeongezeka maradufu kaskazini mwa ukanda huo..
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Tue, 19 Mar 2024 - 11554 - LANDESA yaelezea ni vipi ushiriki wao CSW68 unaleta nuru kwa wanawake Tanzania
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu yale wanayofanya kutekeleza maudhui ya kipaumbele ya mwaka huu ya kumwezesha mwanamke na mtoto wa kike ili hatimaye kupunguza umaskini na kuimarisha usawa wa kijinsia. Shirika la kiraia la kutetea haki ya ardhi kwa wanawake, LENDESA tawi la Tanzania linaloungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake ni miongoni mwa washiriki ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Khadija Mrisho, anayeongoza kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke au Stand For Her Land. Khadija anaanza na kile kilichowaleta.
Mon, 18 Mar 2024 - 11553 - FAO: Baa la njaa lanyemelea Gaza
Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani.
Rein Paulsen, Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Dharura na Mnepo FAO akizungumza hii leo huko Roma, Italia wakati wa kutolewa kwa ripoti hiyo ya uchambuzi wa viwango vya uhakika wa kupata chakula au IPC kwa Ukanda wa Gaza, anasema takwimu zinajenga taswira ya hali ya kutia wasiwasi mkubwa. Na pindi tunapofikiria kuhusu Gaza Kaskazini, ambako hali ni mbaya zaidi, uchambuzi wa sasa unatuonesha kuwa njaa ni dhahiri katika kipindi cha kuanzia sasa na Mei 2024.
Hii ina maana tunapotazama mwelekeo wa takwimu za hali ya upatikanaji chakula na lishe tunaona hali ya kutisha. Kusini, hali nayo imezidi kuwa mbaya na huko tunashikilia makadirio yetu ya uwezekano wa baa la njaa.”
Ripoti inaonesha kuwa mwendelezo wa uhasama umesambaratisha sekta ya kilimo, ambayo familia za Gaza inategemea kwa ajili ya kujipatia kipato.
“Watu wote kwenye ukanda wa Gaza wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu mkubwa wa chakula ukiwekwa katika kiwango cha 3, na 4. Hii inaamanisha nusu ya idadi ya watu wote wa eneo hilo, takribani milioni 1.1 wanaweza kukabiliwa na janga kubwa la ukosefu wa uhakika wa chakula la kiwango cha 5.”
Hivyo amesema usaidizi wa haraka unahitajika kurejesha uzalishaji wa chakula na kwa mujibu wa ripoti
“Inatueleza kuwa baadhi ya mifugo iko hai, na inaweza kusaidiwa na ndio maana FAO inajikita kusaidia mahitaji ya kujipatia kipato Ukanda wa Gaza. Kwa sasa tumepata kibali cha kupeleka tani 1500 za ujazo za chakula cha mifugo.”
Amesema uhai wa mifugo utakuwa hakikisho la upatikanaji wa maziwa kwa familia, maziwa ambayo yatakuwa ni lishe bora kwa watoto na hivyo kukabili utapimlo uliokithiri miongoni mwa watoto.
Akatamatisha akisema, “uhakika wa kupata chakula utawezekana kukiweko na amani. Na haki ya kupata chakula ni haki ya msingi. Hili linapaswa kuzingatiwa na wadau wote.”
Mon, 18 Mar 2024 - 11552 - 18 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa unalowakumba waPalestina katika ukanda wa Gaza, na kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi ya Sudan Kusini. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni?
- Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani.Timu kutoka Kurugenzi ya Haki na Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii akizungumza na Khadija Mrisho, Afisa kutoka shirika la kiraia la kutetea haki ardhi kwa mwanamke LANDESA tawi la Tanzania yeye akiwa kiongozi wa kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke. Akiwa hapa New York, Marekani akishiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, anaelezea kile walichojifunza. Lakini anaanza na kile kilichowaleta.Katika mashinani tutaelekea Ngong nchini Kenya kusikia ujumbe unaotia moyo wasichana waathirika wa mimba za utotoni.
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Mon, 18 Mar 2024 - 11551 - Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wasaidia jeshi la Sudan Kusini kutathmini kesi dhidi ya askari
Timu kutoka Kurugenzi ya Haki Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo.
Tathimini itawezesha kufunguliwa mashtaka kwa askari wa jeshi ambao wanashukiwa kufanya uhalifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia.
Mama Sarah Bennert, mwanaharakati na mwakilishi wa wanawake anasema hatua hii inawakilisha ishara ya haki na uwajibikaji.
"Tuna masuala mengi yanayotukabili hapa kama wanawake. Wakati mwingine unaripoti kesi na haki imechelewa na unabaki kukata tamaa na bila msaada wowote. Sasa, kwa uwepo wa timu ya tathmini hapa chini tunatumai kesi hizo zote walizozizingatia zitasikilizwa kwa sababu baadhi yetu ambao bado tuna kesi tuna kiwewe."
Idrissa Sylvaine ni Mshauri wa haki sheria wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) anasema,
“Tathmini hiyo itasaidia kukuza utawala wa sheria, kuleta haki kwa waathiriwa na kuwawajibisha askari wa SSPDF. Tathmini hiyo pia itachangia katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.”
Mon, 18 Mar 2024 - 11550 - Ushirkiano wa dhati waliotuonesha ulifanya wananchi waachane na mpango wa kuwapiga mawe MONUSCO- Chifu Makofi
Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10) kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.
Mkuu wa TANZBATT-10 Luteni Kanali John Peter Kalabaka amekabidhi bendera ya Tanzania kwa Kamanda wa TANZBATT-11 Luteni Kanali Vedasto Ernest Kikoti ikiwa ni ishara ya kuanza majukumu ya ulinzi wa amani, katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Kamanda wa FIB-MONUSCO Kanali Alex Tamson Malenda.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Luteni Kanali Kalabaka amesema kwenye upande wa operesheni wameweza kukabili na kupunguza mashambulizi yanayofanywa na vikundi vilivyojihami kwenye eneo la ulinzi la TANZBATT-10 halikadhalika kuepusha mauaji ya raia wasio na hatia na pia kuepusha vitendo vya ubakaji.
“Kijamii tumeweza kushirikiana na jamii ya hapa Beni-Mavivi na pia kuwapatia misaada mbali mbali ya kijamii,” amesema Mkuu huyo wa TANZBATT-10.
Luteni Kanali Vedasto Ernest Kikoti ambaye amepokea jukumu la ulinzi akaeleza bayana kuwa watatekeleza majukumu yao vyema kwa kuzingatia taratibu za Umoja wa Mataifa na kwamba watakuwa tayari kuendelea kushirikiana na raia.
“Tunaomba wananchi wakubali na waelewe dhamira hiyo, waukubali Umoja wa Mataifa ili kuupa nafasi uweze kutekeleza wajibu wake wa kulinda wananchi wa DRC,” ameeleza Luteni Kanali Kikoti.
Makofi Bukuka Gervain ambaye ni Chifu wa eneo hilo akashukuru TANZBATT-10 kwa ushirikiano walioonesha wakati wote wa kipind ichao cha ulinzi wa amani Beni-Mavivi na kueleza kuwa Kamanda wa Kikosi hicho alikuwa yuko karibu sana na wanajamii akitolea mfano wakati wa michezo ikiwemo mpira wa miguu.
“Ushirikiano wao na sisi umewezesha raia kufungua nyoyo zao na kuondokana na fikra zao za kupiga mawe MONUSCO barabarani. Sasa barabara zilibaki wazi na MONUSCO wakafanya kazi yao vema,” amesema Chifu Makofi
Meja Fatuma Haruna Makula, wa TANZBATT-11 ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati ya wanajeshi wanawake kutoka Tanzania na wanawake wa Beni-Mavivi akisema, “wanawake maafisa na askari tuliokuja hapa wote tumepita mafunzo mbali mbali kuhusu suala zima la ulinzi wa amani. Tutahakikisha wanashiriki vema shughuli za ulinzi wa mani kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa chini ya MONUSCO.”
TAGS: Amani na Usalama
News: TANZBATT 10, TANZBATT-11
REgion.: Afrika
Focus: DRC
UN/Partner: MONUSCO
Fri, 15 Mar 2024 - 11549 - Wasichana ni majaji watarajiwa, wafuate ndoto zao katika masomo ya Uanasheria - Hakimu Pamela Achieng
Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Majaji Wanawake duniani yalifanyika tarehe 10 Machi 2022, ikiangazia Haki katika Mtazamo wa Kijinsia. Umoja wa Mataifa umeendelea kuadhimisha siku hii kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa wa kijinsia na kushughulikia masuala ya uadilifu wa mahakama yanayohusiana na jinsia. Huku mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa jijini New York Marekani, nchini Kenya Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Redio Domus amekutana na Pamela Achieng, Hakimu katika mahakama ya Ngong iliyo katika Kaunti ya Kajiado ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini kama mwanamke aliamua kuingia katika tasnia hii.
Fri, 15 Mar 2024
Podcasts ähnlich wie Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
- Conversations ABC listen
- Global News Podcast BBC World Service
- El Partidazo de COPE COPE
- Herrera en COPE COPE
- The Dan Bongino Show Cumulus Podcast Network | Dan Bongino
- Es la Mañana de Federico esRadio
- La Noche de Dieter esRadio
- Hondelatte Raconte - Christophe Hondelatte Europe 1
- Dateline NBC NBC News
- 財經一路發 News98
- La rosa de los vientos OndaCero
- Más de uno OndaCero
- La Zanzara Radio 24
- L'Heure Du Crime RTL
- El Larguero SER Podcast
- Nadie Sabe Nada SER Podcast
- SER Historia SER Podcast
- Todo Concostrina SER Podcast
- 安住紳一郎の日曜天国 TBS RADIO
- アンガールズのジャンピン[オールナイトニッポンPODCAST] ニッポン放送
- 辛坊治郎 ズーム そこまで言うか! ニッポン放送
- 飯田浩司のOK! Cozy up! Podcast ニッポン放送
- 吳淡如人生實用商學院 吳淡如
- 武田鉄矢・今朝の三枚おろし 文化放送PodcastQR