Filtrer par genre

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

530 - Fahamu hatua za kuzifikia Sakramenti ya Upadre na majukumu yao.
0:00 / 0:00
1x
  • 530 - Fahamu hatua za kuzifikia Sakramenti ya Upadre na majukumu yao.

    Ungana na Padre Titus Aamigu katika kipindi cha Ujumbe wa Bibilia, mada ni juu ya Sakramenti ya Upadre.

    Wed, 15 May 2024 - 55min
  • 529 - Fahamu namna ya Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam Walivyo jipanga kuimalisha Imani kwa Waamini.

    Karibu uungane na Mtangazaji  Elizabeth Masanja katika kipindi cha Utume wa Walei, Mwezeshaji Padre Vitalis Kasembo Mkrurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo kuu la Dar es salaam ameambatana na Dokta Hellen Makwani Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani, wanaendelea na mada Clinic ya Uongozi.

    Wed, 15 May 2024 - 58min
  • 528 - Fahamu namna ya watu walivyo shiriki kuinjilisha kwa haraka.

    Ungana na Mtanagazaji Fredy William katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi , Mwezeshaji Padre Dominic Mavu, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania, akiendelea kueelezea mada mama ya Injilisha kwa haraka.

    Wed, 15 May 2024 - 55min
  • 527 - Fahamu upendo wa Yesu kwa Binadamu.

    Karibu ungane na Martin Joseph katika kipindi cha Nena Nami Bwana, Mwezeshaji ni Padre Denis Mrimila,  kutoka Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kihesa Kanisa Kuu, Jimbo Katoliki Iringa, leo ananena nasi juu ya Upendo wa Yesu kwa Binadamu.

    Wed, 15 May 2024 - 36min
  • 526 - Fahamu msimamo wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kuhusu ulinzi wa Watoto.

    Ungana na Mtangazaji Happiness Mlewa katika kipindi cha Kutoka Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania, TEC, Mada inayozungumziwa ni juu ya ulinzi wa mtoto, Mwezeshaji Padre Paulino Mlingo, Mratibu kitengo cha ulinzi wa mtoto kutoka  Baraza la Maaskofu Tanzani, TEC.

    Wed, 15 May 2024 - 44min
Afficher plus d'épisodes