Filtra per genere

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

534 - Ni, kwa namna gani Moyo Mtakatifu wa Yesu unainjilisha kwa haraka?
0:00 / 0:00
1x
  • 534 - Ni, kwa namna gani Moyo Mtakatifu wa Yesu unainjilisha kwa haraka?

    Ungana na Erick Paschal, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi studio tupo na Padre Dominic Mavula, Mkurugenzi wa Matangazo ya Radio Maria Tanzania,akizungumzia Injilisha kwa haraka na Moyo Mtakatifu wa Yesu.

    Fri, 17 May 2024 - 53min
  • 533 - Ni, kwanini kikundi cha Karismatiki Katoliki hakikubaliki ndani ya Kanisa?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Daudi Fungameza, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea,  Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kikundi cha Karismatiki Katoliki kilianzishwa na nani? na kwanini kikundi hicho kinaonekana kama hakikubaliki ndani ya Kanisa?

    Fri, 17 May 2024 - 22min
  • 532 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na nne]
    Fri, 17 May 2024 - 49min
  • 531 - Ufahamu utofauti kati ya mwenzi Mei na mwenzi mwingine.

    Karibu Ungane nami Happiness Mlewa, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe, Mkurugenzi wa  Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na  Paroko wa Parokia ya Kaazi Jimbo Katoliki Bukoba ni muendelezo wa mada Faraja ya Imani.

    Fri, 17 May 2024 - 50min
  • 530 - Fahamu hatua za kuzifikia Sakramenti ya Upadre na majukumu yao.

    Ungana na Padre Titus Aamigu katika kipindi cha Ujumbe wa Bibilia, mada ni juu ya Sakramenti ya Upadre.

    Wed, 15 May 2024 - 55min
Mostra altri episodi