Podcasts by Category

Habari RFI-Ki

Habari RFI-Ki

RFI Kiswahili

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

825 - Kila Ijumaa ni fasi yako mskilizaji kuchangia mada ndani ya rfi Kiswahili
0:00 / 0:00
1x
  • 825 - Kila Ijumaa ni fasi yako mskilizaji kuchangia mada ndani ya rfi Kiswahili

    Kila siku ya Ijumaa rfi Kiswahili inakupa mskilizaji nafasi ya changai mada yoyote ambayo unapenda, liwe jambo linalofanyika hapo ulipo au yale umeskia katika taarifa wetu.

    Juma hili pamekuwa na matokeo mengi tu, katika ulingo wa siasan michezo, biashara, usalama na hata mazingira.

    Hii hapa baadhi ya micango yenu.

    Sat, 18 May 2024
  • 824 - Je mataifa tajiri yanaweza saidia mataifa maskini kupambana na

    Wiki hii Paris, ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa Kimataifa kujadili namna ya kuyasaidia mataifa masikini hasa barani Afrika, kufikia malengo ya kukumbatia nishati safi ya kupikia na kuachana na mkaa na kuni.

    Ufaransa, imeahidi kutoa Euro Milioni 100 kusaidia kufikia malengo hayo ndani ya miaka mitano ijayo.

    Unaamini mataifa tajiri yatasaidia Afrika katika hili ?

    Serikali ya nchi yako inafanya nini kukumbatia matumizi ya nishati safi kama gesi ?

    Haya hapa baadhi ya maoni yako.

    Thu, 16 May 2024
  • 823 - Somalia : Yataka ujumbe wa umoja wa mataifa wa kisiasa kuondoka

    Serikali ya Somalia imeandikia bazara la usalama  la umoja wa mataifa ikitaka ujumbe wa umoja huo ambao umekuwa ukisaidia serikali katika maswala ya kisiasa na usalma kuondoka.

    Hakuna sababu maalumu zilizotolewa na serikali ya Somalia, hapa tunakuuliza je ni sahihi kwa ujumbe huu wa umoja wa mataifa  kuondoka kipindi hiki nchi hiyo ikizidi kupitia changamoto za kiusalama?

     

    Haya hapa baadhi ya maoni yako.

    Wed, 15 May 2024
  • 822 - Ujuzi au vyeti, serikali ya Kenya inawasaka wafanyakazi waliotumia vyeti ghushi kupata ajira

    Serikali ya Kenya inaendesha uchuguzi kuhusiana na madai ya baadhi ya wafanyakazi wake kumiliki vyeti ghushi, walivyotumia kupata ajira.

    Unafaikiri mtu anapaswa kuajiriwa kutokana na vyeti  vyake au ujuzi wa kazi ?

    Nchini mwako ajira hutolewa vipi ?

    Haya hapa baadhi ya maoni yako.

    Tue, 14 May 2024
  • 821 - Nini mchango wa masharika ya kirai katika mataifa yetu ya Africa

    Kongamano la kwanza la mashirika ya kiraia la Umoja wa Mataifa limekamilika jijini Nairobi wiki iliyopita, huku wito wa mazungumzo ya uwazi na ukweli kati ya serikali na mashirika hayo ukisisitizwa.

    Upi mchango wa mashirika ya kiraia kwenye nchi zetu?

    Unadhani yamefanya vya kutosha kuzisaidia jamii na kuchochea maendeleo?

    Kipi zaidi kifanyike kuboresha uhusiano kati yake na Serikali?

     

    Ski makala

    Mon, 13 May 2024
Show More Episodes