Filtra per genere

Jua Haki Zako

Jua Haki Zako

RFI Kiswahili

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

270 - Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii
0:00 / 0:00
1x
  • 270 - Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii

    Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica.

     Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au  wale  huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi.

    Kwa mjibu wa twakwimu za shirika la afya duniani WHO ni kwamba wanawake 15 kati ya 100 barani Afrika hawana uwezo wa kupata watoto, na kati ya wanawake 6 angalau mmoja huwa hawana uwezo wa kupata mtoto kidunia.

    Swala la kukosa kupata mtoto hushuhudiwa kati ya wanawake na wanaume, ila hapa barani africa kasumbuka mara nyingi huelekezewa kina mama, hili likisababisa dhiki, unynyapaa, ufukara miongoni mwa wanawake wengi wao sasa wakiathiriwa na afya ya akili na hata kisaikolojia.

    Licha ya tatizo hili kuwa na suluhu, wengi wamesalia kukosa imani kutokana kwani hawana pesa za kutafuta tatibu husika.

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    Tue, 21 May 2024
  • 269 - DRC : Makundi ya waasi yatuhumiwa kwa ukatili wa kijinsia dhidi ya raia mbilimo

    Nchini DRC ; familia ya jamii ya  mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo  wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu.

    Wanawake na wasichana kutoka jamii hii wengi ni waathiriwa wa vitendo vya  ubakaji , vinavyo tekelezwa na wanaume kutoka makundi ya waasi mashariki mwa DRC, visa hivi vina tendwa na wanaume .

    Mwezi Aprili mwaka huu kule mkowani Ituri, watetezi wa haki za binadamu walichapisha ripoti ilioashiria namna wasichana na wanawake mbilikimo , wamebakwa na wanapiganaji wa makundi ya waasi.

    Hali hii imedaiwa kuchochewa na  imani potofu kwamba , ukitenda tendo la ndoa na mwanamke au msichana mbilikimo, huwezi kufariki kwa risasi vitani wala kuambukizwa  baadhi ya magonjwa .

    Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.

    Sat, 18 May 2024
  • 268 - Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?

    Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini  za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume.

    Wajiku Maina raia kutoka nchini Kenya, anasema katika jamii ya leo hakuna anayeshughulikia haki na majukumu ya mtoto wa kiume, hali ambayo imechangia kizazi kizembe cha mtoto wa kiume.

     

    Skiza makala haya kufahamu suluhu kwa baadhi ya changamoto za mtoto wa kiume.

    Thu, 09 May 2024
  • 267 - Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023

     Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi.

    Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika.

    Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha  na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya.

    Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu.

     

    Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.

    Thu, 02 May 2024
  • 266 - Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu

     Unamkumbuka  kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya.

    Baada ya takriban  mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini   waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.

    Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.

    Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi

    Katika haya  mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya  alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa 

    Thu, 25 Apr 2024
Mostra altri episodi