Filtrar por género

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

544 - Je, Ibrahimu alifanya makosa na alitubu?
0:00 / 0:00
1x
  • 544 - Je, Ibrahimu alifanya makosa na alitubu?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Julian Alfons Kidungu, Kutoka Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Takatifu Mdabulo Jimbo Katoliki  Mafinga, swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema Ibrahimu alipozaa na kijakazi baada ya kushauriwa na Sara Mkwee alipona hapati Mtoto.   Je, Ibrahimu alifanya makosa?   Kama alifanya makosa mbona katika Bibilia […]

    Mon, 20 May 2024 - 25min
  • 543 - Je, Skapulari ni alama gani katika Kanisa Katoliki?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Ayubu Polycarp Mwashibili, kutoka Parokia ya  Mtakatifu Yohane Mbatizaji Makongolosi, Swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema nini maana ya Skapulari?

    Mon, 20 May 2024 - 24min
  • 542 - Fahamu madhara ya vidhibiti mimba.

    Ni kwa mara nyingine ninakualika katika kipindi cha Pro – Life utetezi wa uhai, ambapo leo tutajikita kuangazia  hitimisho la mada ya vidhibiti mimba.

    Fri, 17 May 2024 - 49min
  • 541 - Je, waufahamu waraka wa kitume wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo II, heshima kwa wanawake?

    Karibu katika Kipindi cha Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican, Mwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha wa Jimbo Katoliki Moshi, mada anayotufundisha siku ya leo ni Waraka wa Kitume wa Baba Mtakatifu Yohane Paulo II  heshima kwa wanawake.

    Fri, 17 May 2024 - 56min
  • 540 - Ufahamu uhusiano wa Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre na historia ya Nabii Isaya.

    Karibu usikilize Kipindi cha Ujumbe wa Biblia na Padre Titus Amigu, Mtaalamu wa Maandiko Matakatifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Jimbo Kuu la Mwanza, ambapo katika kipindi hiki anaendelea kufafanua juu ya Sakramenti ya Daraja Takatifu ya Upadre, akijikita zaidi katika historia ya Nabii Isaya.

    Fri, 17 May 2024 - 56min
Mostrar más episodios