Filtrer par genre

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

495 - Fahamu kwa kina juu ya Mirathi.
0:00 / 0:00
1x
  • 495 - Fahamu kwa kina juu ya Mirathi.

    Karibu Uungane na Mtanagazaji Elizabeth Masanja katika Kipindi cha Ijue Sheria, Mwezeshaji ni Mh. Hassan Mlanga Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo  Bomani Iringa Mjini, Mada inayozungumziwa ni juu ya Mirathi.

    Fri, 03 May 2024 - 50min
  • 494 - Ni, kwanamna gani Maandiko Matakatifu yanatualika Kuinjilisha kwa haraka ?

    Karibu Ungane nami Erick Paschal, katika kipindi cha Katekisimu Katoliki Shirikishi Mwezeshaji ni Padre Deodatus Katunzi Kagashe Mkurugenzi wa Matangazo wa Radio Mbiu Sauti ya Faraja Kagera na  Paroko wa Parokia ya Kaazi  Jimbo Katoliki Bukoba.    Mada ni Injilisha kwa haraka.

    Fri, 03 May 2024 - 57min
  • 493 - Fahamu juu ya muendelezo wa Uzao wa Adam na Hawa.

    Karibu Uungane na Mtangazaji Happiness Mlewa katika Kipindi cha Maswali ya Imani, Mwezeshaji ni Frateri Ayuto Kogwa kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho – Jimbo kuu la Songea, Swali linalojibiwa linahoji juu ya kabla ya Adam na Hawa je, kulikuwa na watu wengine?

    Fri, 03 May 2024 - 29min
  • 492 - Ni, Kwanini Wakatoliki tunapokea Mwili wa Kristo katika Umbo la Mkate tuu?

    Karibu katika kipindi cha Maswali yahusuyo Imani na Frateri Peter Mjwauzi, kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho Jimbo kuu la Songea swali la Msikilizaji linalojibiwa linasema kwanini sisi Wakatoliki tunapokea mwili wa Kristo katika umbo la Mkate tuu na wakati wa Sala ya Ekaristi Padre anasema twaeni mnywe wote?

    Mon, 29 Apr 2024 - 28min
  • 491 - Fahamu mambo unayotakiwa kufanya unapoingia Kanisani hadi inapoisha Misa Takatifu.

    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea. Leo Frateri Elikana Nyagabona anajibu swali lililoulizwa, naomba kujua ninapoingia Kanisani ni mambo gani natakiwa kufanya hadi inapoisha Misa Takatifu?

    Fri, 03 May 2024 - 27min
Afficher plus d'épisodes