Podcasts by Category

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

Haraka sana ilienea kote Italia, tayari katika miaka ya 90, uzoefu huu wa kipekee wa redio uliamsha shauku katika sehemu zingine za ulimwengu. Baadaye, kila mara chini ya uelekezi na usaidizi wa Radio Maria Italia, Radio Maria nyingine iliibuka Amerika (kuanzia na Peru), Afrika (kwanza Burkina Faso), sehemu nyingine za Ulaya… na hivyo Familia ya Ulimwengu ya Radio Maria ilizaliwa mnamo Juni 1998, na kuwa NGO inayotambuliwa na UN, yenye makao makuu ya kisheria huko Roma. Madhumuni yake ni kuendeleza mradi wa kimisionari, kujibu maombi yanayotoka katika maeneo yote ya dunia, kuhakikisha uhalisi wa chapa, kutoa usaidizi wa kiufundi kwa RM zote, na kukuza mabadilishano na usaidizi kati ya kila redio. Familia ya Ulimwengu inadumisha mahusiano ya mara kwa mara ya taarifa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya Kijamii la Kiti Kitakatifu

501 - Zifahamu Sheria za Ekaristi Takatifu.
0:00 / 0:00
1x
  • 501 - Zifahamu Sheria za Ekaristi Takatifu.

    Karibu uungane na Raymond Karega katika kipindi cha Sheria za Kanisa, kwa namna ya kipekee Padre Ladsilaus Mgaya, Mwanasheria wa Sheria za Kanisa kutoka Jimbo Katoliki Njombe, anazungumzia sheria za Ekaristi Takatifu.

    Sun, 05 May 2024 - 52min
  • 500 - Fahamu Uraibu wa tabia ya uongo.

    Ungana na Happiness Mlewa katika kipindi cha Uraibu, muwezeshaji ni Padre Richard Matanda Tesha, kutoka Jimbo Katoliki Moshi, mada anayozungumzia ni tabia ya uongo.

    Sun, 05 May 2024 - 57min
  • 499 - Fahamu uhusiano wa utandawazi na wito wako.

    Karibu ungane na Martin Joseph katika kipindi cha Fahamu Wito Wako, Muwezeshaji ni Padre Innocent Bahati Mushi, kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, Jimbo Kuu la Arusha, mada anayozungumzia ni mambo ya utandawazi.

    Fri, 03 May 2024 - 47min
  • 498 - Amka na Mama Pasaka [Sehemu ya kumi na mbili]
    Fri, 03 May 2024 - 50min
  • 497 - Je, Mei mosi ni sikukuu ya Kikanisa au ya Kiserikali?

    Karibu katika kipindi cha Maswali Yahusuyo Imani, kutoka seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino Peramiho, Jimbo Kuu la Songea, na Frateri Jackob Venusto Mkandawile anajibu swali lililoulizwa je, Mei mosi ni sikukuu ya Kikanisa au ya Kiserikali, na kwanini Mtakatifu Yosefu aliwekwa msimamizi wa Wafanyakazi?

    Fri, 03 May 2024 - 29min
Show More Episodes