Podcasts by Category

Gurudumu la Uchumi

Gurudumu la Uchumi

RFI Kiswahili

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

224 - Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu
0:00 / 0:00
1x
  • 224 - Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu

    Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.

    Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.

    Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.
     

    Thu, 11 Apr 2024
  • 223 - Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma

    Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.

    Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.

    Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.

    Mon, 04 Mar 2024
  • 222 - Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake

    Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.

    Mon, 04 Mar 2024
  • 221 - Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi

    Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.

    Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji.

    Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.

    Mon, 04 Mar 2024
  • 220 - Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu

    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu.
     

    Mon, 04 Mar 2024
Show More Episodes